MAKAO MAKUU YA MKOA MPYA WA SONGWE KUBAKIA MKWAJUNI

MAKAO MAKUU YA MKOA MPYA WA SONGWE KUBAKI MKWAJUNI



Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa Mbeya akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya wakimsikiliza mkuu wa mkoa Mbeya akiongea na waandishi wa habari


Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya hatimaye yatoa ufafanuzi na kupigilia Msumari maamuzi ya Kamati ya Ushauri (RCC) ya kupeleka Makao makuu ya Mkoa mpya Mkwajuni Wilayani Chunya.
Akitoa maamuzi ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa Mbeya akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake amesema Kamati imeridhika na ushauri uliotolewa na Kamati ya Ushauri iliyofanyika Julai 4, Mwaka huu.
Kandoro amesema lengo la kukutana na kamati ya ulinzi na usalama ni kutokana na kuibuka kwa maneno toka kwa baadhi ya Wananchi ambao wanadai maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya kupeleka Makao makuu ya Mkoa Mpya Mkwajuni Wilayani Chunya hayakuzingatia vigezo vya umbali wa baadhi ya maeneo.
Amesema katika kuliletea ufafanuzi jambo hilo Mkuu huyo wa Mkoa alidai kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ushauri wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri na Wenyeviti wao wameitwa ili kutoa maelezo kwenye kamati ya Ulinzi kama endapo mapendekezo yaliyotolewa na RCC hayakuzingatia matakwa ya wananchi.
Ameongeza kuwa baada ya Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa kuridhika na maelezo ya wajumbe hao imebariki na kuamua kuwa mapendekezo ya Kamati ya Ushauri yabaki vile vile kwa Mkoa mpya kuwa Songwe inayotokana na Mto Songwe uliopita kila Wilaya zinazounda Mkoa huo ambazo ni Momba, Mbozi, Chunya na Ileje.

Na Mbeya yetu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.