Mkenya Wanyama asajiliwa na Southampton


Victor Wanyama
Southampton imemsajili mcheza kiungo wa Celtic Victor Wanyama kwa kitita cha pauni milioni kumi na mbili na nusu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye alijiunga na Cletic kutoka kwa klabu ya Beerschot ya Ubelgiji mwaka wa 2011, amesaini mkataba wa miaka minne na Southampton.
Wanyama, kutoka Kenya, aliteuliwa kuwa mchezaji bora mchanga katika ligi ya Scottland mwaka uliopita na alifunga bao wakati wa mechi yao ya kuwania kombe la klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Barcelona ambayo Celtic iliibuka na ushinda wa goli moja kwa bila.
Kiasi hicho ndicho cha juu zaidi kwa mchezaji yeyote kuuzwa nchini Scottland.
Wanyama vile vile amevunja rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoma Kenya kushiriki katika ligi kuu ya Premier ya England.
Kwingineko Swansea imekamilisha usajili wa Wilfreid Bonny kutoka kwa klabu ya Vitesse arnhem ya Uholanzi kwa kitita cha pauni milioni kumi na mbili kiwango ambacho ndicho kubwa zaidi kwa klabu hiyo kumnunua mchezaji yeyote.
Hata hivyo usajilki huo utategemea ikiwa mchezaji huyo atapewa kibali cha kufanya kazi nchini England.
Bonny ambaye alikuwa amesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya uholansi, alifunga magoli 21 baada ya kucheza mechi 30 msimu uliopita pekee.
Klabu ya Westham vile vile ilikuwa imewasilisha ombi la kutakakumsajili mchezaji huyo kutoka Ivory Coast lakini Swansea ikafanikiwa kwa kutoa kiasi cha juu.vic

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.