MSHAMBULIAJI WA HEARTLAND YA NIGERIA ATUA DAR USIKU HUU KUJIUNGA NA YANGA SC

Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 16, 2013 SAA 7:52 USIKU
SIKU chache baada ya Simba SC kumsaini mfungaji wa bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Amisi Tambwe wa Vital’O ya Burundi, wapinzani wao wa jadi, Yanga SC wamejibu mapigo.
Mshambuliaji wa Heartland FC, moja ya timu tishio Afrika, Ogbu Brendan Chukwudi ametua usiku huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kusaini Mkataba wa kuchezea mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC.
Chukwudi alitua majira ya saa 6:00 usiku kwa ndege ya shirika la Kenya (KQ) na akatumia saa nzima kwa taratibu za Idara ya Uhamiaji ili kuingia nchini, kabla ya kupokewa na Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako aliyeongozana na Meneja, Hafidh Saleh  na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.   
Kifaa hicho; Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako (kushoto) akiongozana na mshambuliaji wa Heartland ya Ligi Kuu ya Nigeria, Ogbu Brendan (kulia) baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, usiku huu kwa jili ya kuja kusaini kuichezea mabingwa hao wa Tanzania Bara. 

Baada ya kutua JNIA, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, aliiambia BIN ZUBEIRY kwamba msimu uliopita alifunga mabao 14 katika Ligi Kuu ya Nigeria na mwaka jana aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, lakini hakupata nafasi ya kucheza kutokana na wachezaji wa Ulaya kupewa nafasi zaidi.
Alisema kabla ya kuja Yanga, alikuwa Misri ambako aliitwa na klabu moja iliyotaka kumsajili, lakini kutokana na vurugu za kisiasa zinazoendelea nchini humo sasa akaamua kuondoka kuja Tanzania kufuata wito wa Yanga SC.


Twende Jangwani; Mwalusako akiondoka na Brendan


Anatoka naye JNIA


Bwana mdogo tu Brendan
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Abdallah Bin Kleb aliiambia BIN ZUBEIRY baadaye kwamba mchezaji huyo wamekuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu na hadi kumleta nchini wameridhika naye ni bora.
“Huyu ni bora, anajua kufunga, ni kijana mdogo na uwezo mkubwa sana. Aliitwa timu ya taifa ya Nigeria, kitu ambacho kwa nchi kama ile yenye wachezaji wengi wazuri kinaashiria huyu ni mchezaji mzuri sana,”alisema.
Kleb alisema kwamba awali walikata tamaa ya kumpata mchezaji huyo baada ya kuitiwa dau nono Misri, lakini imekuwa bahati yao amekwepa machafuko huko na kuamua kuja kufanya kazi Tanzania.  
Kleb alisema watamkabidhi kwa kocha Mholanzi, Ernie Brandts mchezaji huyo kabla ya kusaini naye Mkataba ili amuone na kutoa baraka zake.
Nchini Nigeria, vyombo vya habari vinamsifu Brendan kama mshambuliaji kinda mwenye nguvu, kasi, uwezo wa hali ya juu na ufundi pia. Klabu ya Esperance Sportif ya Tunisia ilijaribu kumsajili msimu huu kujiongezea nguvu katika kampeni zake za kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini pande hizo mbili zikashindwa kufikia makualiano.


Anapakia mizigo kwenye gari


Safari Jangwani
Ni hatari mno anapoingia kwenye eneo la hatari na ana kipaji cha hali ya juu cha kufunga kwa kichwa na miguu yote- na ni mmaliziaji mzuri.
Mshambuliaji huyo alijiunga na Heartland msimu uliopita akitokea Enugu Rangers, aliyoanza kuichezea mwaka 2008. Kisoka Ogbu aliibukia Unth Enugu, kabla hajajiunga na Enugu Rangers.
Brendan aliifungia mabao 11 Enugu Rangers na kuwa mfungaji bora wa klabu katika Ligi Kuu  msimu wa 2010/2011 na akaihama klabu hiyo, akiwa ameifungia jumla ya mabao 30 kwenye mashindano yote.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji wapya walioitwa na kocha Stephen Keshi katika kikosi cha Nigeria, kiliochokwenda kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini pamoja na Tony Okpotu wa Lobi Stars, Mannir Ubale wa Kano Pillars na Fidelis Saviour, aliyekuwa FC Taraba kabla ya kuhamia Enyimba. 
Keshi alijumuisha wachezaji 15 wanaocheza Ulaya katika kikosi hicho, akiwemo kiungo wa Chelsea, John Mikel Obi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Liberia mjini Calabar, Oktoba 13, mwaka jana.
Kikosi hicho kilikuwa; Makipa: Chigozie Agbim (Warri Wolves) na Daniel Akpeyi (Heartland). Mabeki: AzubuikeEgwuekwe (Warri Wolves), Papa Idris (Kano Pillars), Godfrey Oboabona (SunshineStars), Umar Zango (Kano Pillars), Solomon Kwambe (Sunshine Stars), BasseyEzekiel (Lobi Stars) na Kingsley Udoh (Heartland)
Viungo: EjikeUzoenyi (Enugu Rangers), Sunday Mba (Warri Wolves), Gabriel Reuben (KanoPillars), Henry Uche (Enyimba), Christian Ofili (ABS), Solomon Jabason (AkwaUnited), Philip Asuquo (3SC) na Gomo Onduku (Sharks).
Washambuliaji: FidelisSaviour (FC Taraba), Sanusi Sani (Gombe United), Izu Azuka (Sunshine Stars), Brendan Ogbu (Heartland), Tony Okpotu (Lobi Stars) na Mannir Ubale (Kano Pillars).
Kama atasajiliwa Yanga, Ogbu atakamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu, wengine wakiwa ni beki Mbuyu Twite (Rwanda), kiungo Haruna Niyonzima (Rwanda) nqa washambuliaji Didier Kavumbangu (Burundi) na Hamisi Kiiza (Uganda).
Lakini Kiiza amemaliza Mkataba wake Yanga, ingawa ameitwa na tayari yupo nchini kwa ajili ya kuonegza Mkataba.
Hapana shaka- Chukwudi anaweza kuwa kiu ya jibu kwa mashabiki wa Yanga juu ya safu yao ya ushambuliaji- bada ya kuonekana wazi msimu uliopita inahitaji mkali wa aina yake, kutokana na wachezaji waliopo sasa kushindwa kuichumia klabu mabao ya kutosha.
WASIFU WAKE: 
JINA: Ogbu Brendan Chukwudi
KUZALIWA: Aprili 7, 1993
UREFU: 1.85M
UZITO: 78KG
NAFASI: Mshambuliaji
KLABU ZA AWALI: Unth Healers F.C, Rangers
International F.C (Mabao 11 katika Ligi, 6 WAFU, 10 Kombe la FA)
KLABU YA SASA: Heartland Fc Owerri. (Mabao 14 katika Ligi, 3 CAF  na 3 Kombe la FA).
MAFANIKIO: Ubingwa mara mbili wa Jimbo Kombe la FA, nafasi ya 3 Kombe la FA Taifa mwaka 2010, nafasi ya 3 WAFU mwaka 2011, bingwa Kombe la FA mwaka 2012 na Mchezaji Bora (MVP) wa Kombe la F.A mwaka 2012.
Mkali wa mabao atua Jangwani

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.