MTOTO ANG'ATWA AJERUHIWA KWA KUNG'ATWA MENO NA MAMAKE

Terethia Fidelis aliyebeba mtoto mgongoni akisindikizwa na umati wa watu toka ofisi ya mkuu wa mtaa alipokuwa akihijiwa kuhusu tuhuma yake ya kumpiga, kumpasua kichwani na kumng'ata na meno mgongoni mtoto wake Magge Fred 8. (PICHA NA JOHN BANDA)

Na John Banda, Dodoma
MTOTO Magge Fred 8 amejuruhiwa kichwani na kung'atwa kwa meno Mgongoni na mabegani na Mama yake mzazi kwa sababu aliiba fedha na kununulia Chips bila ruhusa.
Magge alisema anajisikia maumivu makali kichwani na mgongoni baada ya kupigwa na mama yake mzazi kutokana na madai ya yeye kutomwambia Dada yake alipo na chips ambazo mama yake alizikuta chini ya mvungu wa kitanda

tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jumanne hii, inadawa kuwa Theresia Fidelis ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo alimpiga na kumjeruhi mwanae, mwandishi wetu alishuhudia kovu kichwani la kipigo cha kitu kilichomchana na huku mgongoni kukiwa na majeraha kadha ya meno ambavyo vimemsababishia maumivu makali.

Akiongea mbele ya Mwenyekiti wa mtaa mama wa mtoto huyo alisema aliamua kumpiga kiasi hicho kutokana na mtoto huyo kumfichia siri Dada yake na pia kuiba fedha ndani na kununua chipsi pamoja na matumizi mabaya ya anasa.
Theresia alisema imekuwa ni kawaida kwa mtoto wake huyo Magge Fred 8  kutosema Dada yake alipo na fedha zinazopotea ndani kutojulikana aliyechukua badala yake anaona chipsi na vitu vingine vidogo vidogo vya anasa ndiyo sababu ya kumpiga vibao mpaka kujigonga ukutani na kuchanika kichwani na kumng'ata kutokana na hasira.
.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume kata ya Mnadani Matwiga Kyata alisema tukio hilo lililpofikishwa ofisini kwake aliamua kuchukua hatua za kisheria na baada ya mahojiano aliamua kuwaita polisi ili sheria ikachukue mkondo wake zaidi.
Baadhi ya akina mama waliokuwepo ofisini hapo kushuhudia tukio hilo walisema mtoto huyo alikimbia toka kwa nyumbani kwao usiku huku akilalama kutaka kuuawa ndipo waka mpeleka kwa mwenyekiti, pamaja na kulaani kitendo alichofanya mwanamke mwenzao.
''We acha hivi unajua uchungu tunaoupata wakati wa kujifungua? kama kweli aliupata angeweza kufanya hivi mpaka kufikia kumng'ata meno akitaka kumnyofoa nyama mtoto wake wala haiingii akili labda akapimwe akili la sivyo achukuliwe hatua kali zinazostahili'', alisema Mwatum Rashid.
Polisi walithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi wanapoona watoto wakifanyiwa vitendo viovu na wazazi au walezi  wao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.