ROMA WATAKA KUIBOMOA ARSENAL YENYEWE IKIHAHA KUJIJENGA UPYA
IMEWEKWA JULAI 17, 2013 SAA 10: 06 JIONI
KLABU ya Roma imetoa ofa ya Pauni Milioni 6.9 kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Gervinho. 
Lyon pia inamtaka mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 26, ambaye hajakwenda kwenye ziara ya kujiandaa na msimu na klabu yake Asia na wanaweza kumtoa mchezaji wao, kiuno Yoan Gourcuff waende London katika sehemu ya dili hilo.
Gourcuff, mwenye umri wa miaka 27, anataka kuondoka na Arsenal inamtaka kiungo huyo. 
One in, one out? Roma want Gervinho but a Lyon offer including Yoan Gourcuff could tempt Arsenal
One in, one out? Roma want Gervinho but a Lyon offer including Yoan Gourcuff could tempt Arsenal
Mmoja nje, mmoja ndani? Roma inamtaka Gervinho, lakini Lyon inamtaka pia na ofa yao inamhusisha pia kiungo Yoan Gourcuff ambaye Arsenal wanamtaka

Wakati huo huo, Chelsea imeonyesha nia ya kumsajili mchezaji anayetakiwa kwa muda mrefu na Arsenal, Gilbert Imbula, mwenye umri wa miaka 20, wa Guingamp, kama Paris Saint-Germain na Roma. 
Beki wa zamani wa Arsenal, Sebastien Squillaci, mwenye umri wa miaka 32, amejiunga na Bastia.
Tayari imeripotiwa Atletico Madrid inataka kumsajili kwa Pauni Milioni 17.5, nyota mwingine wa Arsenal, Santi Cazorla.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Miguel Angel Gil Marin alikuwa London jana usiku kujaribu kukutana na Arsenal kwa ajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28.
Atletico ina fedha za kutosha baada ya kumuuza Radamel Falcao klabu ya Monaco Pauni Milioni 51 na wanafikiri Pauni Milioni 17.5 zitamfanya Arsene Wenger awape Cazorla.
Ambitious bid: Atletico Madrid will offer Arsenal £17.5million for Santi Cazorla
Anatakiwa: Atletico Madrid itaipa Arsenal ofa ya Pauni Milioni 17.5 kwa ajili ya Santi Cazorla

Wakati Wenger na karibu kikosi chake chote kipo ziarani Vietnam, Cazorla hayupo, baada ya kupewa muda zaidi wa kupumzika kufuatia kuwa na timu yake ya taifa kwenye Kombe la Mabara. 
Marin alitarajia kuzungumza Dick Law, Ofisa wa Arsenal anayeshughulika na uhamisho wa wachezaji na ambaye pia hajaenda ziara ya Mashariki ya mbali na timu.
Atletico ilitaka kumsaini Cazorla msimu uliopita kutoka Malaga, lakini haikufika dau la Pauni Milioni 16.5 ambalo Arsenal walitoa. 
Superstar: Cazorla made a phenomenal impact in his first season at Arsenal, contributing 12 goals and 16 assists
Super Star: Cazorla alifanya vizuri Arsenal katika msimu wake wa kwanza, akifunga mabao 12 na kutoa pasi 16 za mabao

Lakini baada ya kumnasa rafiki mzuri wa Cazorla, David Villa kutoka Barcelona, klabu hiyo ya Hispania inataka kujiimarisha zaidi.
Hakuna hakika kama Arsenal itakubali kumuuza mmoja katika ya wachezaji bora kwa sasa- Cazorla aliyefunga mabao 12 na kutoa pasi 16 za mabao msimu uliopita. 
Wenyewe wanataka kuimarisha kikosi chao kwa kuwasajili Luis Suarez au Gonzalo Higuain, na si kupoteza nyota wake kama miaka iliyopita, lakini Atletico wana matumaini fedha itazungumza.
Wanted: Luis Suarez is wanted by Arsenal, though the £40million price tag could put them off
Anatakiwa: Luis Suarez anatakiwa na Arsenal, ingawa dau la Pauni Milioni 40 linaweza kuwarudisha nyuma

Wakala wa Suarez amesema  dau la kuuzwa mchezaji huyo ni kuanzia Pauni Milioni 40 ambaye inafahamika hafurahii maisha Liverpool na Arsenal ilikuwa tayari kutoa Pauni Milioni 35. 
The Gunners pia inaweza kujaribu bahati yake kwa Wayne Rooney ambaye inaonekana ana shaka ya kuwasilisha barua ya maombi ya kuondoka Manchester United, ingawa anatakiwa pia na Chelsea iliyoonyesha nia ya dhati ya kumng'oa Old Trafford.
Arsenal inajiandaa kucheza mechi nyingine katika ziara yake Vietnam leo.
Investing in a Spanish Villa: David Villa (second right) trains with his new Atletico Madrid team-mates
Uwekezajaji kwa Mspanyola Villa: David Villa (wa pili kulia) akifanya mazoezi wenzake katika timu mpya, Atletico Madrid

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI