SOMA TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAUAJI YA MFANYAKAZI WA MGODI WA TANZANIE, KITALU C, MIRERANI WILAYANI SIMANJIRO

Tarehe 20 Julai, 2013 kulitokea mauaji ya mfanyakazi wa mgodiwa Tanzanite ulioko kitalu

 C, Mirerani wilayani Simanjiro kwakupigwa risasi na mchimbaji kutoka mgodi wa wachimbaji wadogowa kitalu D katika eneo hilo.


Kitendo hicho kimetokana na wachimbaji wadogo wanaopakanana Kitalu C kuvuka mipaka ya vitalu vyao na kuendesha uchimbajindani ya Kitalu C, jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Madiniya Mwaka 2010 na Kanuni zake.

Kwa sasa Kitalu C kinamilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Madinila Taifa (STAMICO) na Kampuni ya Tanzanite One kwa asilimia 50kwa 50. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika. 
Wizara imesikitishwa sana na mauaji hayo ambayo ni ukiukwaji wataratibu za usalama migodini.

Serikali haitavumilia kuona 
vitendo hivyo vikiendelea nakuhatarisha usalama wa wachimbaji katika migodi ya TanzaniteMirerani.

Tunapenda kuwatangazia 
wamiliki wa migodi yote ya wachimbajiwadogo katika vitalu B na D ambayo uchimbaji wake unafanyikandani ya mipaka ya Kitalu C kuwa wasitishe shughuli zao mara mojana wahakikishe kuwa uchimbaji unafanyika ndani yamipaka ya vitalu vyao.

Aidha, uchimbaji uzingatie taratibu za usalama migodini ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na utumiaji wa silaha za aina yoyote migodini. Ukaguzi wa migodi kubaini
migodi  inayoendeshauchimbaji ndani ya mipaka ya kitalu C utafanywa na Timu yawataalam wa Wizara ya Nishati na Madini. Vitalu vitakavyobainika kuhusika leseni zake zitafutwa na uchimbaji utatakiwa kusitishwakatika migodi hiyo.

IMETOLEWA NA,

WIZARA YA NISHATI NA MADINI
26 JULAI, 2013

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.