WATEJA SABA WA TIGO WAIBUKA WASHINDI WA PROMOSHENI YA 'MILIKI BIASHARA YAKO'

 Meneja Bidhaa wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Husn Seif (kushoto) akibofya kwenye kompyuta  kumpata mmoja wa wateja saba  walioshinda Bajaji katika droo ya kwanza ya Promosheni ya 'Miliki Biashara Yako' iliyofanyika Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja wa Chapa ya Tigo, William Mpinga na Mkaguzi kutoka Bodi ya Taifa Kusimamia Michezo ya Kubahatisha, Bakar Maggid.
                                                  Wanahabari wakichua habari hiyo
Mpinga akimpigia simu mmoja kati ya washindi saba akimjulisha kwamba ameshinda

 Dar es Salaam, Julai 29, 2013 – Tigo Tanzania leo imefanya droo yake ya pili katika promosheni yao kabambe iitwayo “Miliki Biashara Yako” na kupata washindi wapya 7 wa wiki iliyopita ambapo kila mmoja alijishindia Bajaji mpya yenye thamani ya Tsh 6,700,000.

Washindi hao ni………
1.Nicolus Maliyatabu Sanga-mkazi Dsm(43)
2.Julius Dilikwije -mkazi wa Same
3.Isabellah edward Msemo(24)-dsm
4.Eliasa Hamisi Mbano(48)Tabora
5.Charles benedect Kato(41) -kinyerezi
6.Evelyn Elisalia Massawe-(22)mwanafunzi mkazi wa kimara
7.Khalidi Jafary Gomani(27)-dsm…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………....

Akizungumza katika mkutano na wanahabari waliohudhuria droo hiyo, Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga aliwapongeza washindi hao na kutoa rai kwa wateja wengine pia kushiriki katika promosheni hiyo.

“Kila mteja wa Tigo anao uwezo wa kujishindia Bajaji moja kila siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh 1,000 tu kwa siku. Ili kuhakikisha kuwa wateja wengi wanafurahia promosheni hii, mteja hahitaji kuweka vocha ya Tsh 1000 kwa mkupuo mmoja ili kushiriki, anaweza kuongeza salio kidogo kidogo hadi kufikisha kiasi cha Tsh 1000 kwa siku na kuweza kuingia kwenye droo. Vile vile mteja anaweza kuongeza salio mara nyingi awezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kujishindia Bajaji. Pamoja na hayo, ili kuwapatia urahisi zaidi wateja, bado mteja anaruhusiwa kuongeza salio pitia namna zote zile ikiwemo Tigo Rusha, Tigo Pesa au kwa vocha ya kawaida,” alisema Mpinga.

“Leo Tigo imetimiza tena kwa hatua ingine jukumu letu tulionao katika kuboresha na kugusa maisha ya Watanzania, kwa kuwapatia nafasi ya kumiliki biashara yao wenyewe kupitia promosheni hii ya “Miliki Biashara Yako”. Hii ni nafasi yakipekee ambapo wateja wetu wanapatiwa fursa ya kuwa wajasiriliamali, kujipatia kipato, kutoa ajira, pamoja na kutoa huduma ya usafiri wenye gharama nafuu kwa jamii.”

Promosheni hii inayalenga kuwainua wateja wake kiuchumi kwa kuwapatia fursa ya kushinda usafiri wa Bajaji 60 kwa muda wa miezi miwili ambapo kila siku mteja atajishindia Bajaji moja.

“Tunaamini kwamba promosheni hii itawapatia wateja wetu sababu nyingine yakutabasamu. Wateja 60 watakaopatikana washindi watajinyakulia Bajaji mpya kabisa ambapo wataweza kuzitumia kuanzisha biashara zao wenyewe. Biashara ya Bajaji ni biashara yenye faida sana, kwa siku mmiliki wa Bajaji anaweza kuingiza kipato cha kati ya Tsh 25,000 mpaka Tsh 30,000 kwa siku, sawa na Tsh 900,000 kwa mwezi, ambayo ni Tsh 10,800,000 kwa mwaka,” alielezea Mpinga.

Bw. Mpinga alisema kwamba kila Bajaji ina thamani ya Tsh 6,700,000. “Tayari Tigo imechukua jukumu la kulipia leseni ya barabara (road license) na bima ya Bajaji. Kwahiyo mteja atakuwa amebakiwa na jukumu la kuja kuchukua Bajaji yake na kuanzisha biashara yake mara moja,” alimalizia Mpinga.
Wiki iliyopita, Tigo ilifanya droo yake ya kwanza katika promosheni hii na kupata washindi watatu ambao tayari wameshakabidhiwa Bajaji zao katika hafla maalum iliyofanyika Soko Kuu, Kariakoo, wiki iliyopita.
KUHUSU TIGO:
Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka 1994 na inapatikana katika mikoa ishirini na sita (26)
Tanzania bara na visiwani.
Lengo la Tigo ni kuwa mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania kwa wateja wake wote ambazo zinaendana na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti za bei nafuu, vifurushi vya intaneti vyenye kasi kubwa na huduma bora za fedha za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.
Tigo ni sehemu ya kampuni kubwa ya <http://www.millicom.com/> Millicom
International Cellular S.A (MIC) ambayo ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi  kwa zaidi ya wateja milioni 43 katika masoko 13 barani
Afrika na Amerika ya Kusini.
"Tabasamu upo na Tigo"
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Amani Nkurlu – Meneja Mahusiano
+255 658 870 107 au +255 712 223 839
 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.