JK AREJEA KUTOKA ZIARA YA CANADA,MAREKANI


Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda huku Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilali akiangalia wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo, akitokea Marekani katika ziara ya kikazi. (PICHA NA IKULU)



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete arejea nyumbani kutoka Canada na Marekani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amerejea nchini mchana wa leo, Jumatatu, Septemba , 2013, baada ya ziara ya kikazi yenye mafanikio makubwa katika Marekani na Canada.
Miongoni mwa shughuli nyingine nyingi katika ziara hiyo, Rais Kikwete alihutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York.
Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini Jumapili ya Septemba 15 alianzia safari yake mjini San Francisco, Marekani, ambako miongoni mwa mambo mengine alizindua Ubalozi Mdogo wa Tanzania katika Jimbo la California.
Rais pia alikutana na kuzungumza na Jumuia ya Watanzania katika Jimbo hilo na kukaribishwa katika Jiji la Vallejo katika sherehe za miaka 20 za uhusiano wa kimji kati ya Jiji hilo na mji wa Bagamoyo.
Ziara ya Rais Kikwete San Francisco ilifuatiwa na ziara ya mjini Washington ambako shughuli zake kubwa zilikuwa kukutana na viongozi wa Bunge la Marekani na pia kuhudhuria Hafla ya Chakula cha Usiku cha Taasisi ya Kulinda Hifadhi na Mazingira ya Bunge la Marekani (ICCF) ambako alitunukiwa tuzo maalum za Mtunzaji Mazingira Bora wa Mwaka.
Aidha, Rais Kikwete alishuhudia utiaji wa saini mikataba ya kufungua Ofisi Ndogo za Ubalozi wa Tanzania katika majimbo mbali mbali ya Marekani.
Baada ya hapo, Rais Kikwete alikwenda Canada ambako alitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Sheria na Chuo maarufu na kikongwe cha Canada cha Guelph ambacho ni maarufu duniani kwa shughuli na utafiti wa kilimo.
Kufuatia ziara hiyo ya Canada, Rais Kikwete alikwenda New York ambako alikuwa na shughuli nyingi ikiwa ni pamoja na kuhutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la UN Ijumaa ya wiki iliyopita, akakutana na Katibu Mkuu wa UN Mheshimiwa Ban Ki Moon, akashiriki kikao maalum cha wakuu wa nchi kujadili hali ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kilichoitishwa na Mheshimiwa Ban Ki Moon.
Akiwa mjini New York, Rais Kikwete pia alikuwa kiongozi pekee wa Afrika aliyealikwa kushiriki katika Mkutano wa Rais wa Marekani Mheshimiwa Barack Obama na taasisi zisizokuwa za kiserikali duniani na pia alihudhuria Halfa Maalum iliyoandaliwa na Rais Obama alipomaliza kuhutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la UN.
Aidha, Rais Kikwete alishiriki Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Clinton Global Initiative na pia akawa mzungumzaji rasmi katika Mkutano wa Kupambana na Ujangili Duniani uliotishwa na Rais Ali Omar Bongo Ondemba wa Gabon.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

30 Septemba, 2013

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI