MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AWASILI MKOANI RUKWA KUSHIRIKI IJITIMAI YA KIMATAIFA

Makamu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya aliopowasili leo tarehe 29 Septemba 2013 katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga kwa ajili kushiriki na kufunga Ijitimai ya Kimataifa inayofanyika Mkoani Rukwa. Ijitimai ni Semina ya kiislam inayolenga kuihamasisha jamii kumcha Mungu kwa kufanya matendo mema na kuacha maovu na machafu.
Kiongozi wa maandalizi ya Ijitimai ya kitaifa na kimataifa inayofanyika Mkoani Rukwa Amir Ali Jumanne akimtambulisha Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam walioshiriki katika maandalizi ya Ijitimai.  
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini CCM, Aeishi Hillal akiteja jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima wakati wa mapokezi ya Makamu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimsomea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad taarifa ya Mkoa wa Rukwa katika Ikulu ndogo ya Sumbawanga. 
Makamu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akizungumza mara baada ya kusomewa taarifa ya Mkoa wa Rukwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya. Katika mazungumzo yake ameshukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na kuupongeza Mkoa wa Rukwa kwa uzalishaji mkubwa wa chakula nchini ambapo ameutaka uongozi wa Mkoa kujikita zaidi kutafuta masoko ya mazao yanayozalishwa na wakulima. 
Ameutaka pia uongozi wa Mkoa kulipa kipaombele suala la usalama akitolea mfano yaliyotokea nchini kenya na kuvitaka vyombo vya dola kuimarisha uhusiano na wanachi katika kuboresha taarifa za ulinzi shirikishi. Aliwaasa pia wanachi kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo nchini kwa kuweka pembeni tofauti zao za kidini na kusaidia kutoa taarifa inayoashiria uvunjifu wa amani kwa vyombo vya dola .
Akizungumzia kongamano la uwekezaji lililofanyika Mkoani Rukwa mwaka jana ameutaka uongozi wa Mkoa kujitangaza zaidi katika fursa zinazopatikana za uwekezaji na kufuatilia wawekezaji waliotoa ahadi za kuwekeza Mkoani Rukwa na kuwawekea mazingira mazuri ya kuwekeza. 
Baadhi ya viongozi wa dini na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar walioongozana na Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad. Katikati ni Waziri wa Habari wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Said Ali Mbarouk. Wengine ni Chief Kadhi wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis na Imam Sheikh Mziwanda Ngwali.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI