Saini zakusanywa kumng’oa Makinda
Na Sharon Sauwa,Mwananchi
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
“Si kweli kwamba Kamati ya Bajeti inalipwa fedha za
ziada kila wakati, hapana, ni pale tu wanapoomba malipo hayo kutokana na
sababu ambazo lazima Spika aridhike nazo. Ieleweke kuwa siyo kamati
hiyo tu, kwa sasa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ambayo inachambua
miswada mingi nayo imekuwa ikiomba na baada ya Spika kuridhia basi nao
wanapewa,”
Akizungumzia suala hilo, Dk Kashililah alisema
Serukamba pamoja na wabunge wengine kadhaa waliteuliwa na Spika kwa
ajili ya kuongeza nguvu katika kamati hiyo wakati wa kipindi cha Bajeti
Kuu ya Serikali.
Aliwataja wabunge wengine walioteuliwa kushiriki
katika Kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa ni John Cheyo (Bariadi
Mashariki-UDP), Salahe Pamba (Pangani - CCM) na Hamadi Rashid Mohamed
(Wawi - CUF).
Kanuni za Bunge
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge katika toleo la
mwaka 2007, kifungu cha 137(1), ili kumwondoa Spika madarakani, mbunge
anayetaka kuwasilisha hoja hiyo atatakiwa kuwasilisha taarifa ya
maandishi ya kusudio hilo kwa Katibu, akieleza sababu kamili ya kutaka
kuleta hoja hiyo.
Kifungu kidogo cha pili kinasema baada ya kupokea
taarifa ya maandishi ya kusudio la kumwondoa Spika kwenye madaraka,
Katibu atapeleka taarifa hiyo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka
ya Bunge kwa ajili ya kujadiliwa.
Kifungu cha tatu kinabainisha kuwa endapo kamati
hiyo itaridhika kuwa zipo tuhuma mahususi dhidi ya Spika zinazohusu
uvunjaji wa masharti ya ibara husika za Katiba, sheria au kanuni
zinazoongoza shughuli za Bunge, basi kamati hiyo itaidhinisha hoja hiyo
ipelekwe bungeni ili iamuliwe.
Kanuni zinasema Naibu Spika, atakalia Kiti cha
Spika wakati wa kujadili hoja ya kutaka kumwondoa Spika madarakani na
Spika atakuwa na haki ya kujitetea wakati wa mjadala na kwamba ili
kumwondoa zinahitajika kura zisizopungua theluthi mbili ya idadi ya
wabunge wote.
source:mwananchi
Comments