JAMII IMETAKIWA KUTUMIA VYAKULA VINAVYOPATIKANA KATIKA MAZINGIRA YANAYOWAZUNGUKA KUBORESHA AFYA ZA FAMILA ZAO

DSC_0494
Afisa kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Valerian Vitalis Kidole, akiendesha mafunzo ya siku nne ya wanahabari na watangazaji wa redio jamii yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO yaliyofanyika katika ukumbi wa Kartasi uliopo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Na Mwandishi wetu.

Wito huo umetolewa na Afisa kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Valerian Vitalis Kidole katika semina ya siku nne kwa waandishi wa habari na watangazaji wa redio jamii iliyomalizika mwishoni mwa katika ukumbi wa Kartasi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Kidole alisema kuwa ili kuhakikisha jamii inapata lishe haina budi kutumia vyakula vile vinavyopatikana katika maeneo wanamoishi kuliko kusubiri vyakula vya msaada kutoka serikalini na vyakula kutoka viwandani.

Hayo yamezungumzwa katika mafunzo ya Kupunguza Madhara ya Maafa na kutoa Msaada wa Dharura yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO kwa ajili ya waandishi wa Habari na watangazaji wa redio jamii yanayofanyika Kahama wakati mwezeshaji akitoa mada ya Usalama wa Chakula nchini.
DSC_0482
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa chakula hutoa msaada wa chakula kwa wananchi pale kunapotokea upungufu wa chakula katika maeneo husika.

Aidha Kidole amesema kuwa chakula cha msaada kinachotolewa na serikali ni nafaka ambayo hayawezi kuboresha afya zao. Katika halmashauri za mikoa nchini ambazo zina upungufu wa chakula, viongozi wa ngazi husika hawana budi kuwaelimisha wanachi juu ya kulima mazao mengi yanayohimili hali ya hewa husika na kwa wakati mwafaka ili kupunguza tatizo la upungufu wa chakula katika maeneo yao. Ni kwa namna hiyo jamii itaipunguzia serikali mzigo wa kutoa chakula cha msaada na badala yake kufanya shuguli nyingine za maendeleo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI