KIFUSI CHAUA WATU WATATU KATIKA MACHIMBO YA KOKOTO JIJINI DAR ES SALAAM
Kuhusu wachimba kokoto waliofukiwa na kifusi Dar mchana wa leo april 4.
Inasemekana
watu watatu waliotambuliwa kwa majina ya Msagala,Jacob na Mhando ambao
ni wakazi wa Bunju jijini Dar es Salaam wamefariki dunia mchana wa
April 04 baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba kokoto.
Watu hao walikua wakichimba kokoto hizo kwenye machimbo ya Mtanzania mwenye asili ya Kiasia aliyefahamika kwa jina la Kara Arjan machimbo yaliyopo eneo la Bunju-Mbweni Dar es salaam.
Taarifa inasema kuwa machimbo hayo yalishapigwa marufuku kutokana na watendaji wake kufanya kazi katika mazingira hatarishi ambapo wachimbaji hao wakiwa kazini,sehemu ya machimbo hayo iliporomoka na kuwafukia.
Picha za kwenye tukio ambazo zinaonyesha pia juhudi za watu wakiendelea na uokoaji pamoja na miili ya watu waliopoteza maisha.

Comments