KINANA AKAGUA MPAKA WA TANZANIA NA BURUNDI.

Katibu Mkuu wa CCM,Kinana akiwa na viongozi wengene wakiangalia jinsi watanzania wanavyopata taabu na kunusurika kifo kwa kuvuka kwenye Mto Malagalasi wakitokea kuuza bidhaa zao na kununua mahitaji mengine katika Soko Buhinja, Kijiji cha Mrambi, Mkoa wa Makamba nchini Burundi. Wananchi hao kutoka Kijiji cha Kibande na vijiji viongine wilayani Buhigwe, Kigoma Tanzania, huenda Burundi kufanya biashara kutokana na upande wa Tanzania kutokuwepo na soko kunakosababishwa na kodi nyingi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni mpaka wa Tanzania na Burundi, alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma,Kinana yupo katika ziara ya siku 5 mkoani humo ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.
 Hizi ni baadhi ya picha zinazoonesha jinsi wananchi wa Tanzania wakivuka mto huo na wengine kuvushwa kwa malipo, wakirudi Tanzania baada ya kufanya biashara upande wa Burundi. 
 Watu wote hao wakisubiri kuvushwa kwenye mto huo Malagalasi,kwa kimtumbwi kimoja ama kubebwa kama baadhi ya picha zinavyoonyesha
Baadhi ya Wanahabari pichani Kulia Bakari Kimwanga kutoka gazeti la Mtanzania na Bwana Jongo kutoka gazeti la Uhuru wakionja joto ya kuvushwa kwenye mto wa Malagalasi ambao ndio sehemu ya mpaka kati ya Burundi na Tanzania.Kuonja adha hiyo hulipia kiasi cha fedha shilingi 500 mpaka 1000 kama nauli.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo kwa msisitizo na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Buhigwe,Kaondo Julius walipokwenda kukagua  mpaka wa Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
Msanii wa kikundi cha ngoma za utamaduni kutoka Burundi wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Kibande, Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.
Mbunge wa Jimbo la Manyovu wilaya ya Buhingwe,Mh.Albert Obama Ntabaliba akizungumza na Wanakijiji cha Kibande,kwenye mkutano wa hadhara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kibande,kwenye mkutano wa hadhara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa chama cha CNDD-FDD,Mkoa wa Makamba nchini Burundi,Bwa.Nishimwe Zen,kabla ya mkutano wa hadhara kufanyika katika kijiji cha Kibande,wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
Wanachama waliohamia chama cha CCM wakionesha kadi zao ambazo walimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM,na kukabidhiwa kadi mpya za CCM.
Sehemu ya Wanachama wapya waliojiunga na CCM,wapatao zaidi ya 300 wakila kiapomara baada ya mkutano wa hadhara kufanyika katika kijiji cha Kibande,wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Mnanila-Manyovu wakishangilia jambo wakati katibu MKuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Mnanila-Manyovu
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mnanila-Manyovu .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Kamati ya Siasa Wilaya ya Buhingwe na kupata taarifa mbalimbali za maendeleo.
Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Buhigwe,Kaondo Julius pamoja na Afisa Mipango,Charles Mduma wakitoa ufafanuzi mfupi kwa Waandishi wa habari kuhusiana na taarifa ya Maendeleo ya Wilya ya Buhingwe iliyotolewa kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Manyovu-Wilaya ya Buhigwe.Mh Albert Obama,mara baada ya kumaliza kikao cha siasa cha wilaya 
Baadhi ya Wakazi wa Buhigwe wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowasili wilayani humo mkoani Kigoma.
Ndugu Kinana akizungumza jambo na baadhi ya Wananchi wa Buhingwe huku wakimsilikiza kwa makini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.