Liverpool leo wanawategemea Suarez, Sturidge na Sterling!



1_e9ea3.jpg

Na Olle Bergdahl Mjengwa,
Hii ni wikendi ya fainali. Jana Arsenal walishinda mechi yao dhidi ya Wigan katika nusu fainali ya kombe la FA. Mechi hii ilikuwa muhimu sana kwa Arsenal, ni kwa kuwa timu hiyo sasa ina nafasi kubwa ya kushinda taji lao la kwanza tangu mwaka 2005!
Lakini, leo Liverpool inacheza mechi dhidi ya Manchester City katika uwanja wa nyumbani wa Liverpool, Anfield. Ni kweli kwamba mechi hii ni kwenye ligi, lakini, mechi hii pia ni kama fainali. Mshindi leo atakuwa na nafasi kubwa kushinda ligi kuu ya Uingereza!
Liverpool wanaendelea kuishangaza dunia ya soka na kwa sasa wameshinda mechi tisa mfululizo katika ligi! Katika uwanja wao wa nyumbani Liverpool wametisha msimu huu. Katika uwanja wa Anfield ,Tottenham walifungwa magoli manne kwa bila, Everton walifungwa kwa magoli manne kwa bila, na Arsenal walifungwa magoli matano kwa bila!
Liverpool wameonyesha kwamba wana uwezo mkubwa wa kufunga magoli mengi dhidi ya timu nzuri wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani. Kwa sasa wengi wanaamini kwamba Real Madrid wana washambuliaji bora duniani. Naongea kuhusu Bale, Benzema na Cristiano Ronaldo. Wachezaji hawa wamepata jina la utani BBC! Lakini katika ligi ya England naamini Liverpool wana washambuliaji bora. Ni Sterling, Sturidge, na Suarez.
Liverpool hawangeshika nafasi ya kwanza bila wachezaji hawa. Liverpool hawana mabeki bora katika ligi kuu. Huwezi kuwalinganisha Skrtel na Sakho na Cahill na Terry wa Chelsea. Kuna timu nyingi ambazo zimeweza kufunga mabao dhidi ya Liverpool. Katika mechi nne za mwisho za Liverpool katika ligi, timu tatu zimefanikiwa kufunga mabao dhidi ya Liverpool, na kwa ujumla, Liverpool wamefungwa magoli sita katika hizi mechi nne!
Lakini, katika mechi hizi nne Liverpool pia wamefanikiwa kufunga magoli kumi na nne! Na ndio maana timu hiyo bado iliweza kushinda mechi hizi. Bila shaka timu hiyo ingepoteza pointi nyingi kama washambuliaji wao hawangefunga magoli mengi. Leo naamini kwamba Man City watakuwa na uwezo wa kufunga mabao dhidi ya Liverpool, lakini, kama Sterling, Suarez na Sturidge wapo katika hali yao ya kawaida kimpira , basi, Liverpool wana nafasi kubwa kushinda mechi hii!
Olle,
Stockholm.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.