Mkurugenzi
wa Utawala na Masoko kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Stanley
Mahembe akiwatambulisha wageni walioketi meza kuu (hawapo pichani)
wakati wa kufunga mafunzo ya Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini,
mafunzo hayo yamefungwa jana Mkoani Morogoro.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera akiwahutubia
Wasimamizi na Wadadisi (hawapo pichani) muda mchache kabla ya kufunga
mafunzo ya Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini, mafunzo hayo
yamefungwa jana Mkoani Morogoro.
Baadhi
ya Wasimamizi na Wadadisi wa Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini
wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel
Bendera (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Zoezi hilo jana
Mkoani Morogoro.
Mgeni Rasmi Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na maofisa wa Serikali pamoja na Wasimamizi wa Zoezi la
Uorodheshaji wa Viwanda nchini mara baada ya kufunga mafunzo ya zoezi
hilo jana Mkoani Morogoro. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)
Comments