TASAF YAANZA HATUA ZA KUTAMBUA KAYA MASIKINJI KATIKA MIKOA YA DODOMA,SINGIDA,KIGOMA,NA KATAVI.

 Mtaalamu kutoka TASAF Makao makuu Bi. Mercy Mandawa mwenye miwani na kompyuta mpakato akiandika baadhi ya mambo yaliyojitokeza kwenye mafunzo ya wawezeshaji ngazi ya wilaya mjini Dodoma.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya namna ya kuendesha kazi yautambuzi wa kaya masikini ngazi ya halmashauri ya wilaya wakimsikiliza mtoa mada hayupo pichani katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Dodoma.
 Mtoa mada katika mafunzo ya wawezeshaji ngazi ya Wilaya, Bw. Andrew Kibona akitoa mada kwenye mafunmzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya Dodoma.
Washiriki wa mafunzo ya uwezeshaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika manispaa ya Dodoma wakimsikiliza mtoa mada hayupo pichani juu ya namna ya kuzitambua kaya masikini .

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,TASAF uimeanza  utekelezaji wa Mpango wa  kunusuru kaya masikini katika mikoa ya Dodoma, Singida ,Kigoma na Katavi ambako mafunzo kwa wawezeshaji wa Mpango huo ngazi ya halmashauri za wilaya yameanza kutolewa.

Mpango huo utakaotekelezwa nchini kote kwa awamu, tayari umekamilika katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambako kaya masikini zitaanza kupatiwa ruzuku kwa ajili ya kuboresha afya kwa mama wajawazito na watoto wenyer umnri wa  chini ya miaka 5, na kuziwezesha kaya husika kumudu gharama za elimu na matibabu kwa familia husika ili kuboresha maisha yao.

Ruzuku hiyo ya fedha pia  inakusudiwa kuzijengea uwezo kaya masikini ziweze kuinua kipato  kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi kulingana na mazingira ya eneo husika ili hatiomaye ziweze kuondokana na umasikini wa kipato.

Akizungumza katika mkutano wa wawezeshaji ngazi ya taifa  mjini Dodoma, Bi Mercy Mandao amehimiza umuhimu wa kuendesha zoezi zima la utanmbuzi wa kaya masikini kwa uangalifu mkubwa ili hatimaye walengwa waweze kupatikana na kuondoa uwezekano wa kuwaacha walengwa kutokana na kutozingatia vigezo maalumu ambavyo huwekwa na wananchi wenyewe kwenye maeneo yao.


Zifiatazo ni picha za baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wawezeshaji  katika manispaa  ya Dodoma yaliyoanza leo Jumanne . Mafunzo kaya hao yatolewa pia katika halmashauri zote za mikoa ya Singida, Kigoma, Katavi, Rukwa ,na Dodoma

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.