WANAFUNZI WATATU WAPOTEZA MAISHA WAKIOGELEA

 


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Kinondoni, linamshikilia mfanyabiashara jijini Dar es Salaam, Mboka David (44) mkazi wa Kijitonyama kwa kosa la kusababisha vifo vya watoto watatu wa shule ya msingi na wengine saba kujeruhiwa walipokuwa wakiongelea katika bwawa la kuogelea ‘Swimming pool’ la Hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi Beach jijini humo  



Taarifa za awali kuhusu tukio hilo ambalo lilitokea  Jumapili Aprili 27, mwaka huu saa 11 jioni katika hoteli hiyo zilidai mwanamke huyo ambaye sasa anahojiwa, aliwachukua watoto wake wakiwa na watoto wengine (wakiwemo waliokufa) kutoka majumbani mwao eneo la Kijitonyama karibu na Polisi – Mabatini bila ruhusa ya wazazi na kuelekea katika eneo hilo.

Habari  zaidi zinaarifu  kuwa, wakati wa tukio mama huyo akiwa na familia yake na watu wengine walikuwa wakijipatia kinywaji (pombe) ndipo watoto hao walipokuwa wakiogelea walizidiwa na maji na kupiga kelele ili kuomba msaada bila kupata mwitikio wowote na hata hapakuwa na mhudumu wa hoteli katika bwawa hilo huku wengine wakifanikiwa kujiokoa wenyewe.


source:mpekuzi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI