Idadi ya wahamiaji yaongezeka Libya

wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika
Mamlaka nchini Libya imesema kuwa imeshindwa kudhibiti idadi ya wahamiaji wanaotaka kuingia Ulaya kwa kutumia mlango wa nyuma.
Inadaiwa kuwa zaidi ya raia laki tatu wamo nchini Libya wakitaka kuvuka bahari ya Mediterenean.
Walinzi wa pwani ya Libya wameiambia BBC kwamba wamepata miili zaidi baharini, ya watu ambao wamepoteza maisha yao kwa kutaka kuvuka bahari hiyo.
Wale wanaokamatwa wakitaka kuanza safari hiyo huwekwa katika jela ndogo ambazo zimejengwa katika pwani ya bahari hiyo.
Mwandishi wa BBC katika mji wa bandari ya Misrata amesema kuwa Libya sasa ndio mlango wa raia wa afrika kuingilia Ulaya.
Muungano wa Ulaya umeonya kuwa mwaka 2014 utakuwa na wahamiaji wengi watakaowasili katika fukwe za mataifa ya Ulaya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI