GARI LA NAIBU WAZIRI MAKALLA LATOLEWA MKUTANONI CHINI YA ULINZI MKALI WA POLISI BAADA YA KUZUKA VURUGU

Gari lililombeba Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, likilindwa na polisi lililopokuwa linaondoka baada mkutano wa hadhara kuvunjika kulikosababishwa na vurugu ambazo waziri alidai kuwa zilipangwa kwa makusudi na wafuasi pamoja na viongozi wa Chadema waliokuwa wakirumbana na viongozi wa CCM, katika Kata ya Goba, Kinondoni, Dar es Salaam jana. Makalla alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Kwa habari zaidi juu ya sakata hilo tembelea blog hii. PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Na Richard Mwaikenda

NAIBU Waziri wa Maji, Amos Makalla, ametolewa kwenye mkutano huku akilindwa na ulinzi mkali wa polisi, baada ya kutokea vurugu jukwaani alizodai zilipangwa mapema kwa makusudi  na viongozi wa Chadema kuvuruga mkutano wake na wananchi katika Kata ya Goba, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

Baada ya kuona vurugu zinazidi eneo hilo la mkutano, viongozi wa Jeshi la Polisi na CCM waliamua kumshauri Naibu Waziri Makalla kuondoka jukwaani na kumsindikiza kwenda kwenye gari ambalo lilikuwa limeegeshwa nyuma ya jukwaa kuu.

Vurugu zilianza mapema jana asubuhi kwa wafuasi wa Chadema na CCM, kurumbana kuanzia mkutano uliofanyika Kata ya Makongo na zilizidi kupamba moto katika mkutano huo wa  Kata ya Goba, ambapo polisi walijitahidi kuutuliza bila mafanikio.

Asilimia kubwa ya wafuasi wa vyama hivyo waliokuwa wakisababisha vurugu, ni wale waliokuwa tangu jana wakisafirishwa kwa magari kutoka eneo moja kwenda lingine, tofauti na wenyeji waliokuwa wanakutwa kwenye mikutano ambao walionekana kuwa watulivu.

Mzozo uliotokea jukwaa kuu na kusababisha Waziri Makalla aondeke, ni marumbano ya kiongozi gani wa vyama hivyo alikuwa anastahili kukaa jukwaani na nani hastahili. Kata hiyo inaongozwa na Diwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Theresia Kihota.

Katika mzozo wa jukwaa kuu, ulichangiwa pia na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema), Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee Pia wa Chadema, waliojitosa katika marumbano hayo dhidi ya viongozi wa CCM, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge na wengineo.

Wakati vurugu zikiendelea jukwaa kuu, uwanjani nako kulikuwa na marumbano makubwa kati ya wafuasi wa vyama hivyo, kiasi cha wengine kufikia hatua ya kupigana. Mshereheshaji alijitahidi kutumia kipaza sauti kuwasihi kuacha lakini ilishindikana.

Akizungumza muda mfupi, kabla ya kuondoka eneo hilo, baada mkutano huo kuahirishwa, Naibu Waziri wa Maji, Makalla, alisema kuwa amesikitishwa kutokea kwa vurugu hizo ambazo alidai kuwa zilipangwa kwa makusudi tangu jana na viongozi wa Chadema kwa lengo la kumvurugia ziara yake.

"Mpango huo tuliujua tangu jana kwamba viongozi wa Chadema wamekula njama za kunifanyia vurugu kwenye mikutano yangu, tabia ambayo si nzuri, kwani tunawanyima haki wananchi taarifa sahihi za utekelzaji wa Ilani ya CCM juu ya upatikanani wa maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ifikapo Septemba, mwaka huu, kutokana na upanuzi wa Bomba la Maji la Ruvu Chini kukaribia kukamilika."Alisema Makalla huku akiingia ndani ya gari na kuondoka akisindikizwa na polisi.

Wakati Makalla akiondoka, eneo hilo la mkutano, alionekana Mbunge wa Ubungo, Mnyika akiwakusanya wananchi na wafuasi wa chama hicho kwa lengo la kuwaeleza jambo, lakini hata hivyo aliambulia kuzungumza na wafuasi wachache wa chama hicho waliokuwa na mabango ya kuidhihaki CCM na Serikali.

Akizungumza na wanahabari pamoja na wafuasi hao, Mnyika alisema ili kuepusha mitafaruku kama iliyotokea tangu juzi kwenye ziara hiyo, si vizuri ziara za kiserikali kuchanganya na za vyama.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.