LICHA YA ARGENTINA KUSHINDA 1-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI, MESSI AKIRI USWISI `KISIKI CHA MPINGO`
Uswizi mmh! Messi, Angel Di Maria na Ezequiel Lavezzi wakishangilia ushindi kwenye chumba cha kubadilishia nguo.
LIONEL Messi amekiri kuwa Argentina walibanwa sana kabla ya Angel Di Maria kufunga bao pekee dhidi ya Uswisi katika dakika za nyongeza lililowapa tiketi ya kwenda robo fainali ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
"Wote tulihangaika, tulihangaika na kuhangaika,' alisema Messi. "Tulianza kuwaza kama haitatokea. Lakini mwisho bahati ilituangukia na tunatakiwa kutumia faida hiyo kusonga mbele".
"Kama ilivyokuwa kwa wote, niliumia sana kwasababu sikufunga. Tulijua kama tungefanya kosa moja tungerudi nyumbani. Hatukutaka kusubiria penati. Tulitaka kumaliza dakika za kawaida".
Mashabiki bab kubwa!: Mpenzi wa Messi, Antonella Roccuzzo na mtoto wao wa kiume Thiago wakitazama ushindi wa Argentina.
Mpe busu hili baba yako: Messi mdogo akipata busu kutoka kwa mama yake baada ya baba yake kutengeneza bao la ushind.
Comments