NEC YAWAPIGA MSASA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSU MABORESHO YA DAFTARI LA KUDUMU WAPIGA KURA KWA KUTUMIA MASHINE ZA KIBALOJIA ZA BIOMETRIC (BVR)


 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia), akifafanua jambo wakati wa mkutano na viongozi wa vyama vya siasa wa kuelezea maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Dar es Salaam .Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Tume hiyo, Jaji John Mkwawa na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa akilalamika kuhusu utaratibu usiofaa ulioandaliwa na NEC wa kuionesha na kuielezea mashine yenye teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR) itakayotumika katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajia kuanza Septemba, mwaka huu. Kutoka kulia ni Katibu wa Oganaizesheni wa CCM, Mohammed Seif Khatib, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam juzi,  kuhusu mfumo mpya wa maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura baada ya kuhudhuria mkutano viongozi wa vyama vya siasa ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuelezea maandalizi ya maboresho hayo.
 Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lisu akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam , akiulalamikia mfumo mpya wa kibailojia wa maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wa Biometric Voter Registration (BVR).
 Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, baada ya kuhudhuria mkutano viongozi wa vyama vya siasa ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuelezea maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Moja ya mashine za kibailojia aina ya Biometric Voter Registration (BVR), zitakazotumika katika uboreshaji wa daftari hilo. Registration (BVR)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.