Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Bw. Stima Kabikile (katikati) akimkaribisha rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia) wakati alipofanya ziara yake ya siku moja katika Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke kwaajili ya kupata taarifa kuhusu kodi za majengo na utendaji kazi wa wataalam wanaoshughulikia masuala hayo na mbinu za kuboresha namna ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia walipaji kodi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya (kulia) Ilala akimsomea taarifa ya makusanyo ya kodi za majengo na mikakati yake ya kufikia malengo waliojipangia ili kuongeza mapato Mhe. Waziri wa Fedha Bi. Saada Mkuya wakati wa ziara ya siku moja katika Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Yusuph Mwenda (kulia) akitoa maelezo yake kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) wakati wa mkutano na viongzoi wa Manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Yusuph Mwenda (kulia) akitoa maelezo yake kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) wakati wa mkutano na viongzoi wa Manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia) akiongozana na viongozi wa Manispaa ya Kinondoni wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Manispaa hiyo jana kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu makusanyo ya kodi za majengo pamoja kupeana mikakati mizuri ya kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi walipaji kodi ambao ni wananchi. katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Bw. Yusuph Mwenda na kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw. Photidas Kagimbo (kulia) akisalimiana na Waziri waFedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) mara alipowasili katika ofisi za Manispaa hiyo kwa ziara ya kikazi katika jana kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu makusanyo zikiwemo njia wanazotumia kukusanya kodi za majengo pamoja kupeana mikakati mizuri ya kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi walipaji kodi ambao ni wananchi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia) akihutubia mkutano huku akisisitiza juu ya kujikita zaidi katika kutumia TEHAMA katika kukusanya kodi za majengo kama njia rahisi inayomrahisishia mlipaji kodi kuweza kulipa kodi zake katika vituo vya huduma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya akipitia moja ya taarifa alizopewa na uongozi wa Halmashauri wilaya ya Kiondoni wakati alipofanya ziara yake ya siku moja ofisi hapo.
Comments