JAMAA ALIYECHOMWA MSHALE WA MGONGONI WAKATI WA MAPIGANO YA KUGOMBEA SHAMBA

MAPIGANO yakurushiana mishale,mawe na marungu yanayohusishwa na kugombea ardhi, yameibuka kati ya wananchi wa Kijiji cha  Sirorisimba wilaya ya Butiama na Kijiji cha Mikomariro wilaya ya Bunda mkoani Mara na kusababisha baadhi ya wananchi kujeruhiwa kwa kuchomwa mishale na kukimbia makazi yao.





Tukio hilo limekuja kufuatia madai ya kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa ardhi baina ya vijiji vya wilaya hizo mbili huku ukimya wa viongozi wa wilaya ukitajwa kuwa chanzo cha kuibuka kwa mapigano hayo.



Wakiongea na Blog hii baadhi ya wananchi wa kijiji cha Sirorisimba  wilaya ya Butiama mkoani Mara wamesema mgogoro huo umeanza miaka mingi iliyopita ambapo wananchi kutoka kijiji cha Mikomariro wilaya ya Bunda wamekuwa wakivamia wananchi wa kijiji hicho lakini mpaka sasa hakuna hatua zinazochukuliwa na viongozi wa wilaya hiyo.


Walisema uvamizi wa maeneo makubwa uliofanywa hivi karibuni katika eneo hilo umesababisha mapigano makali na kusababisha mtu mmoja kuchomwa Mshale mgongoni na kulazwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara.


Mmoja wa majeruhi aliyechomwa mshale kwenye tukio hilo na kulazwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara Hamisi Nyahanga amesema  alivamiwa kwenye eneo lake la kilimo na wananchi na kuambiwa siku zake za kuishi zimekwisha na kuamua kukimbia ndipo alipopigwa mshale wa mgongo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:

NI HESHIMA KUBWA SANA KUIFUNDISHA YANGA - KOCHA MPYA WA YANGA

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

”RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI”

KOCHA SEAD RAMOVIC AMRITHI GAMONDI YANGA.

UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE