MTEMVU AAPA CCM KUSHINDA KWA KISHINDO MITAA YOTE TEMEKE UCHAGUZI UJAO WA SERIKALI ZA MITAA

 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto) akiwa na msanii Omar Tego jukwaani wakicheza  katika mkutano wa hadhara uliandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT-CCM) Kata ya Azimio, kwenye Uwanja wa Shule ya Sokoine, Tandika, Dar es Salaam juzi. Alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 45 wa UWT. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wasanii wa kikundi cha hamasa cha CCM Temeke wakitoa burudani ya pekee katika mkutano huo.
 Diwani wa Kata ya Azimio, Khamis Mzuzuri akihutubia na kummwagia sifa lukuki Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu kwa uchapakazi wake.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akihutubia katika mkutano wa hadhara uliandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT-CCM) Kata ya Azimio, kwenye Uwanja wa Shule ya Sokoine, Tandika, Dar es Salaam,  Alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 45 wa UWT. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Kikundi cha hamasa cha CCM Temeke kikishangilia wakati Mtemvu akihutubia
 Mtemvu akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika mkutano huo
 Diwani wa Viti Maalum CCM Temeke, Mariam Mtemvu (katikati) akibadilishana jambo na mmoja wa viongozi wa UWT.
 Baadhi ya viongozi na wananchama wa CCM wakisikiliza kwa makini wakati Mtemvu akihutubia katika mkutano huo.
 Handa Rashid (50) akikabidhiwa NA mTEMVU  kadi ya uanachama wa UWT
 Rehema Salum akipokea kadi ya UWT kutoka kwa Mtemvu
 Mtemvu akimakabidhi kadi ya UWT, Malizia Rajab.
Mtemvu (katikati) akiungana na akina mama kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na msanii wa mipasho Omar Tego baada ya mkutano huo kumalizika.

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ametamba kuwa, CCM itapukutisha kwa kishindo upinzani wote katika jimbo hilo kwa kushinda mitaa yote katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

"Wala hatutatumia nguvu bali tutaichukua mitaa yote hata hiyo michache iliyopo sasa chini ya upinzani, kwa kutumia mtaji wa mafanikio makubwa tuliyoonyesha katika utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi hiki", alisema Mtemvu.

Mtemvu alitoa tambo hizo wakati akihutubia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Jumuia ya Wanawake Tanzania, Kata ya Azimio, kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Sokoine, katika Kata hiyo, Temeke jijini Dar es Salaam.

Alisema, CCM inao uhakika wa kutwaa viti vyote hadi kurejesha vichache vilivyopo sasa chini ya upinzani kwa kuwa mengi ambayo CCM iliahidi kupitia yeye wakati akiomba kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliopita yamefanyika.

Mtemvu alitaja baadhi ya yaliyotekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ambazo karibu zote zimeboreshwa kwa kujengwa kwa kiwngo cha lami tofauti na awali ambapo ilikuwa kero kubwa kwa kuwa zilikuwa hazipitiki kutokana na ubovu tena za vumbi.

"Zamani nilikuwa kila nikisimama jukwaani mnaniolea matatizo na kero lukuki hasa kuhusu hizi barabara, sasa leo hatuzungumzii matatizo ya barabara, tunazungumzia tu sasa kuboresha taa kwenye mitaa na barabara hizi", alisema Mtemvu.

Alisema, kuanzia mwezi huu Septemba, taa zote katika barabara na mitaa kwenye jimbo hilo zitawaka ambapo sasa zinafanyiwa maboresho ili zitumie nishati ya jua (solar) ili kupunguza changamoto ya gharama za malipo ya umeme wa taa hizo.

Mtemvu alisema, kukamilika kwa taa hizo itakuwa janga kwa vibaka ambao wamekuwa wakitumia fursa ya giza kujificha wakati wakivizia kuiba kwenye nyumba za watu na pia kukwapua wapitanjia nyakati za usiku.

Alisema mbali na kuboresha barabara CCM pia kupitia uongozi wake imeweza kuboresha hali za wananchi hasa kina mama na vijana kwa kuviwezesha vikundi vyao vya ujasiriamali kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ambapo sasa zaidi ya vikundi 100 vimenufaika.

Mtemvu aliahidi kuendelea kushirikiana na wabunge wengine wa Temeke na mkoa wa Dar es Salaam kwa jumla kuhakikisha watendaji wabovu serikalini wanakabwa koo ili wawajibike ipasavyo kutumikia wananchi.

Pia aliahidi kuhakikisha anaedelea kupigania kupatikana kwa mazingira bora ya kufanya kazi zao mamalishe na bodaboda kwa kuwa wana mchango mkubwa katika maendeleao ya jamii.

"Najua haiwezekani bodaboda zote zikaingia mjini, lakini tunachofanya ni kupigania kuhakikisha unakuwepo utaratibu mzuri utakaowezesha baadhi kufika mjini bila kuharibu taratibu na sheria zilizopo. Pia Mamalishe kwa kuwa lazima waendelee na shughuli zao tunawatafutia utaratibu bora kufanya shughuli zao kwa amani badala ya kukimzwa kimbizwa na mgambo kila mara", alisema Mtemvu.

Katika mkutano huo, uliosheheni burudani mbalimbali ikiwemo msanii Omari Tego kuimba wimbo maalum wa CCM ambao ulikonga nyoyo za waliohudhuria, Mtemvu aligawa kadi kwa wanachama wapya 45 wa UWT.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI