RAIS KIKWETE AZINDUA BARABARA YA DUMILA-RUDEWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe pamoja na Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua jiwe la msingi kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Sehemu ya barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Ujenzi ambao walikuwa wakisubiri tukio la ufunguzi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kushoto akiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale wakitazama ramani pamoja na picha mbalimbali za barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Mc Mavunde kulia akiwatambulisha watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya ujenzi kabla ya Ufunguzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa
Sehemu ya wakazi wa Dumila waliojitokeza kwa wingi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete licha ya giza kuingia mjini Dumila.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI