Beki wa Simba SC, Issa Rashid 'Baba Ubaya' akimtoka mchezaji wa KMKM |
IMBA
SC imewafunga mabingwa wa Zanzibar, KMKM mabao 5-0 katika mchezo wa
kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara usiku huu Uwanja
wa Amaan, Zanzibar.
KMKM
inayofundishwa na Ally Bushiri ‘Bush’ ambayo Jumatano wiki hii
ilifungwa 2-0 na Yanga SC, leo iligeuzwa asusa na Wekundu wa Msimbazi.
Simba
SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao 4-0, yaliyotiwa kimiani na
Amisi Tambwe mawili, Amri Kiemba na Shaaban Kisiga ‘Malone’ moja kila
mmoja.
Wazito; Kutoka kulia Musley Ruwey, Hans Poppe na Salim Abdallah 'Try Again' |
Amri
Kiemba ndiye aliyefungua karamu ya mabao ya Simba SC hii leo, dakika ya
tatu ya mchezo baada ya kupewa pasi nzuri na kiungo Mrundi, Pierre
Kwizera na kuwatoka wachezaji wawili wa KMKM kabla ya kufumua shuti kali
lililogonga mwamba wa ndani wa lango.
Amisi Tambwe akafuatia dakika
ya 14 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Salim Amour kufuatia yeye
mwenyewe kupiga mkwaju wa penalti, baada ya kiungo, Haroun Chanongo
kuangushwa kwenye boksi.
Tambwe tena akafunga bao la
tatu dakika ya 23 akimalizia krosi maridadi ya Ramadhani Singano ‘Messi’
kabla ya Kisiga kufunga la nne dakika ya 37, kufuatia kazi nzuri ya
Kiemba.
Okwi katikati akiwa na Mosoti kulia na Butoyi kushoto |
Kipindi
ha pili, kocha Mzambia, Patrick Phiri alibadilisha kikosi kizima
akimuacha Nahodha Jopseph Owino pekee na dakika ya 60 Elias Maguri
akahitimisha karamu ya mabao kwa bao safi la tano.
Mshambuliaji
Mganda, Emmanuel Okwi aliyetangaza juzi kurejea Simba SC kutoka kwa
mahasimu, Yanga SC usiku huu alikuwepo, lakini alibaki benchi muda wote
wa mchezo.
Amisi Tambwe na Ramadhano Singano 'Messi' kulia wakishangilia usiku huu Amaan |
Viongozi
wa Simba SC wakiongozwa Makamu wa Rais, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe, Kassim Dewji,
Musley Ruwey, Mohammed Nassor ‘Steven Seagal’, Crescentius Magori, Said
Tuliy na wengineo walikuwepo kushuhudia mchezo huo.
Kikosi
cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda/Hussein Sharrif ‘Cassilas’
dk46/Peter Manyika dk84, Miraj Adam/Abdi Banda dk46/Nassor Mssoud
‘Cholo’dk84, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’/William Lucian ‘Gallas’
dk46/Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ dk84, Joram Mgeveke/Hassan Isihaka
dk46, Joseph Owino, Pierre Kwizera/Abdallah Seseme dk46, Haroun
Chanongo/Twaha Ibrahim ‘Messi’ dk46, Amri Kiemba/Ibrahim Hajibu dk46,
Amisi Tambwe/Elias Maguri dk46, Shaaban Kisiga ‘Malone’/Awadh Juma dk46
na Ramadhani Singano ‘Messi’/Uhuru Suleiman dk46.
KMKM;
Salim Amour, Pandu Hajji, Faki Hamad/Makame Hajji dk30, Juma
Rashid/Nassor Ali dk30, Halfan Khamisi/Mudrik Muhibu dk30, Moka Shaaban,
Ame Khamis, Abdi Kassim ‘Babbi’, Haji Simba/Kassim Nemshi dk30, Maulid
Ibrahim na Khamis Ali.
Comments