Kisima chenye urefu wa futi 50 ambapo mtoto Mack Johnson amefariki dunia baada ya kutumbukia, Mtoto huyo mwenye umri wa miaka (5)alikuwa anasoma darasa la awali katika shule ya Sheer Bliss mtaa wa majengo mapya manispaa ya Shinyanga. Ambapongazi mbili za jeshi la zimamoto pamoja na kuungwa lakini hazikuweza kufikia kina cha kisima hicho na badala yake ikatumika kamba ndefu na mmoja wa wananchi kujitoa mhanga kutumbukia nayo kisimani kuutoa mwili wa mtoto huyo.
Mashuhuda wamesema tukio hilo limetokea leo saa tatu asubuhi ambapo mtoto huyo alitumbukia kwenye kisima hicho wakati akicheza na wenzake karibu na kisima hicho kilichopo eneo la shule ambacho kimefunikwa na makaravati yaliyoonekana kuchakaa.
Mwili wa mtoto Mack Johnson ukitolewa kwenye kisima cha maji na wananchi waliofika eneo la tukio wakishirikiana na jeshi la wananchi na jeshi la zimamoto na uokoaji.
Comments