HABARI MPASUKOOO. VURUGU ZAZUKA KATI YA POLISI NA RAIA ILULA,IRINGA

Ni baada ya Polisi Kuuwa Raia

Inasemekana polisi walivamia eneo la kilabuni na kuanza kupiga kila raia na kusababisa kifo cha huyo mama muuza Pombe za kienyeji. Kosa ni kufungua kilabu cha Pombe kabla ya muda ulioruhusiwa kisheria.

Wananchi wamechoma matairi barabara Kuu hakuna gari inayopita, Polisi bado hawajafika waliopo wamekimbia baada ya kuzidiwa na wananchi.

Sasa hivi wananchi wanaandamana kwenda kuchoma moto kituo cha polisi.

Updated....
Gari tatu zilizosheheni FFU zimewasili mabomu yanapigwa mfululizo, sasa hivi wanasafisha barabara kwa kuzima moto na kutoa matairi njiani.

Wananchi Walioenda kituoni wamechoma moto matairi na magari mabovu yaliyopakiwa kituoni
.


Quote By TEKNOLOJIA View Post
Kituo cha polisi cha Ilula mkoani Iringa kimechomwa na wananchi wenye hasira kufuatia polisi kumuwa mwanamke mmoja mfanyabiashara ya mama ntilie wakati wa msako maalum ulioendeshwa na jeshi la polisi dhidi ya wafanyabiashara hao.Inasemekana wakati wa purukushani za kukimbia ndipo polisi mmoja alimchota mtama huyo mama wakati anakimbia na kusababisha mama wa watu kuanguka na kufariki hapo hapo.

Source: Radio Couds
Quote By dubu View Post
WANANCHI wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo asubuhi kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.

Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.

Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.