JK AWEKA MASHADA YA MAUA KWENYE MAKABURI YA YA MARAIS CHILUBA, MWANAWASA NA SATA ZAMBIA

Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Zambia Michael Sata aliyefariki mwaka jana katika eneo la maziko ya viongozi wa kitaifa jijini Lusaka Zambia leo.Rais Kikwete alitumia  wasaa huo pia kuweka shada la maua katika makaburi ya marais wa Zambia waliofariki Marehemu Frederick Chiluba na Levy Mwanawasa.(PICHA NA FREDDY MARO)


                                TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekwenda Saudi Arabia asubuhi ya leo, Jumapili, Januari 25, 2015, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita.
Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Mjini Berlin, Ujerumani ambako Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili kesho, Jumatatu, Januari 26, 2015, akitokea Riyadh, Saudi Arabia, anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) ambako viongozi mbali mbali duniani watajadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.
Baada ya kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa.
Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania katika Ufaransa na pia nyumba ya balozi.
Rais Kikwete baada ya kumaliza ziara zake za kikazi katika Ujerumani na Ufaransa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

25 Januari, 2015


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI