WAZIRI JUMA NKAMIA AWATAKA WAMILIKIWA WA VYOMBO VYA HABARI KUWAKATIA BIMA WAFANYAKAZI WAO

       

unnamed1
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akijibu swali Bungeni mjini Dodoma.
unnamed2Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandishi Athumani Mfutakamba akisoma taarifa ya kamati hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo bungeni mjini Dodoma.
unnamed3Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo unnamed4Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yaMasuala ya Ukimwi Lediana Mng’ong’o akiwasilisha taarifa ya kamati yake.
unnamed7Baadhi ya wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
unnamed8Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma akiwemo Mbunge wa Morogoro Kusini Dkt. Lucy Nkya (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza.
unnamed9Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mhe. Kapt (Mstaafu) George Mkuchika (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge kwenye mlango wa Bunge mjini Dodoma.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO,Dodoma
…………………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-Maelezo Dodoma
Naibu Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwakatia wafanyakazi wao bima ili ziweze uwasaidia wakati wanapopatwa na madhara wakiza kazini.
Akijibu swali la mbunge wa viti maalum Anna Mallac, kuhusu mpango wa Serikali kuwapatia ulinzi waandishi pale wanapokuwa wakifanya kazi katika matukio hatari, Naibu Waziri Nkamia alisema kuwa serikali inafahamu mazingira ya kazi ya wanahabari na inawajibika kikatiba katika kutoa ulinzi kwa raia wake wote wakiwemo wanahabari.
“Uandishi wa habari ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine muhimu katika jamii kama ilivyo taaluma ya sheria ualimu na udakatari na ni muhimu kufahamu na kuzingatia miiko ya taaluma pale wanapokuwa katika eneo la kazi”alisema Nkamia
Aidha alibainisha kuwa jukumu la kwanza kwa waandishi wa habari ni kujilinda na kujihami wao wenyewe kwa kuwa wanayafahamu mazingira yao ya kazi na pia kuzingatia miiko ya taaluma yao kwa kuangalia wanayotakiwa kufanya na kutofanya katika eneo husika.
Aliongeza kuwa wanahabari wanatakiwa wazingatie sheria bila shuruti kwa kuwa nao ni wananchi kama walivyo wananchi wengine na hakuna aliye juu ya sheria .
Hata hivyo Serikali imekuwa ikiwapatia waandishi wa habari vifaa maalum katika matukio mbalimbali ya kitaifa ikiwemo vitambulisho na mavazi maaalum ya kuwatambulisha wakiwa katika eneo la kazi ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuwalinda na madhara yeyote.
Naibu Waziri Nkamia alieleza kuwa kwa sasa wizara yake imekuwa ikiandaa muswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao utawasilishwa mbugeni wakati wowote kuanza sasa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.