ZANZIBAR MIDIA CORPORATION LTD YAANDA TAMASHA LA WASANII WA ZANZIBAR.


 

 Mwenyekiti wa Tamasha la tunzo za wasanii bora Zanzibar mwaka 2014/15  Seif Mohd Seif akizungumza na waandishi wa habari  juu ya maandalizi ya tamasha hilo  Ofisini kwake mtaa wa Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Picha Na Makame Mshenga –Maelezo Zanzibar.
 Mratibu wa Tamasha hilo Ramadhani Senga akijibu masuala ya waandishi wa habari kuhusu tunzo za mwaka huu katika mkutano uliofanyika Jengo la Zanzibar Media Corporation Limited mtaa wa Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo katika jengo la Zanzibar Media Corporation Limited wakifuatilia mazungumzo hayo.
 Meneja Masoko wa Zanzibar Media Corporation Limited Said Khamis akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari  katika Mkutano wa  maandalizi ya Tamasha la tunzo za wasanii bora Zanzibar mwaka huu uliofanyika jengo la Zanzibar Media Cortporation Limited mtaa wa Mombasa. Picha Na Makame Mshenga –Maelezo Zanzibar.


Na Ramadhani Ali-Maelezo Zanzibar  .            
Taratibu za Tamasha la kuwatafuta wasanii bora wa Zanzibar (Zanzibar Music Awards) zinazosimamiwa na Kampuni ya Zanzibar Media Corporation  inayomiliki kituo cha Zenj Fm radio na kitengo cha Zenj Entertainment kwa mwaka 2014/2015 zimeanza rasmi leo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Zanzibar Media Corporation, mtaa wa Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Tamasha  hilo Seif Mohd Seif amesema maandali yamekamilika. Amesema tunzo hizo ambazo zinalengo  la kuwanyanyua wasanii wa Zanzibar kibiashara zitafikia kilele chake siku ya Ijumaa tarehe 27.2.2015 katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani.

“Lengo la tunzo hizi ni kuweza kuwatangaza wasanii wetu wa hapa Zanzibar kibiashara, kuona thamani ya kazi zao na mchango wa sanaa zao unavosaidia jamii kuipa taaluma kupitia sanaa hizi,” alisisitiza Seif Mohd Seif.

Ameongeza kuwa tamasha la mwaka huu ambalo ni la nane, kama yalivyo matamasha yaliyopita  yanasaidia kuinua sekta ya utalii kutokana na wageni mbali mbali kuhudhuria. Ametoa shukrani kwa wasanii wote wa Zanzibar kwa kuonyesha moyo wa kuziimarisha kazi zao ambazo zinakuwa na mvuto kwa jamii kwa kuendeleza sanaa nchini.

Pia ameipongeza Kamati ya  majaji kwa kazi kubwa waliyofanya ya kupitia kazi za wasanii, na wadau mbali mbali kutoka vyombo vya habari vya Zanzibar ikiwemo Baraza la sanaa kwa michango mikubwa waliyotoa kufanikisha maandalizi ya Tamasha hilo.

Mwenyekiti wa  Zanzibar Music Award amesema katika Tamasha hilo jumla ya makundi 18 yatawania tunzo hizo kwa wasanii wa Zanzibar pekee.
Ameyataja makundi hayo kukwa ni  Video bora ya mwaka muziki wa kizazi kipya, video bora ya mwaka taarab ya kisasa, Mwanamuziki bora wa mwaka wa hip hop, Mwanamuziki wa mwaka wa R&B, Mwanamuziki bora wa Afro pop na Mtaarishaji bora wa mwaka.

Wengine ni Mwanamuziki bora wa kiume  na wa kike taarab ya kisasa, Wimbo bora wa taarab ya kisasa ya mwaka, Mwanamuziki bora wa kiume na wa kike taarab asilia, Mwanamuziki bora wa kike na kiume muziki wa kizazi kipya na wimbo bora wa mwaka wa kizazi kipya.

Katika makundi hayo pia kutakuwa na tunzo ya Mwanamuziki bora chipukizi wa mwaka, Mwanamuziki bora wa mwaka na Mshairi bora wa mwaka. Seif Mohd Seif amewataka watu wote wanaopenda kushiriki tunzo za mwaka huu kuwa upigaji  wa kura umeanza rasmi leo Jumapili na utamalizika siku ya Jumatano tarehe 25.2.2015 na matangazo ya kupiga kura yatarushwa na vyombo mbali mbali na katika Gazeti la Nipe Habari na kupitia website yao www.zenjifmradio.com

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.