Hatimaye
chama cha CHADENA kimeshinda kesi dhidi ya aliyekuwa mwanachama wake
Zitto Kabwe.Mahakama Kuu (Mziray,Judge) amekubaliana na hoja za
wanasheria wa CHADEMA za pingamizi dhidi
ya case hiyo kwamba ilifunguliwa bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Mahakama Kuu imeipa CHADEMA gharama zote za kuendesha case hiyo. Kwa
maana hiyo hakuna shauri lolote Mahakamani kwa sasa kuhusu suala hilo.
Aidha, Mahakama imeamuru Zitto alipe gharama zote za
kesi.
Wanasheria wa chama, Peter Kibatala na John Mallya na Tundu Lisu wanatarajiwa kuongea na Vyombo vya Habari hii leo.
Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili.
Hoja yake ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.
Alidai anataka mahakama iagize kamati kuu ya CHADEMA kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake.