KINANA ATOA USHAURI KWA KATIBU MKUU KIONGOZI KUWASIMAMISHA MARA MOJA VIONGOZI WALIOTAJWA KWENYE SAKATA LA ESCROW

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiiwa amebeba maji kwenye madumu aliposhiriki umwagiliaji maji katika shamba nyanya la vijana wajasiriamali wa CCM katika Kijiji cha Nkulabi, Kata ya Mpunguzi, Jimbo la Dodoma Mjini leo wakati wa ziara yake,mkoani Dodoma juzi.Kinana yupo mkoani Dodoma kwa ziara ya siku tisa ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi pamoja
na kuzitafutia ufumbuzi.
 Komredi Kinana akimwagilia maji zao la nyanya la vijana wajasiriamali wa CCM katika Kijiji cha Nkulabi, Mpunguzi, Dodoma. Kinana aliwapongeza vijana hao wanne kwa kuamua kuanzisha shamba hilo ambalo mzao yake yanawasaidia kujikimu kimasha ambapo aliwataka vijana wengine kuiga mfano huo.
 Komredi Kinana akinukuu mambo muhimu alipokuwa akijadiliana jambo na Viongozi wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu kwenye mkutano na wanafunzi wa vyuo vilivyopo Dodoma leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Christopher Ngubiagai na Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa Mkoa wa Dodoma, Steven Lwitiko.
 Mwanafunzi wa Chuo cha CBE-DodomaThomas Mathias akitoa ushauri kwa Serikali kuanzisha mfuko mwingine wa kusaidia kusomesha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanaokosa mkopo wa elimu.

 Komredi Kinana akizungumza na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kwenye Ukumbi wa NEC, Mjini Dodoma
 Nape akielezea jinsi Serikali ilivyowasaidia vijana watano wasomi waliobuni mradi wa kisasa wa kuosha magari, ambapo Serikali imewapatia mtaji wa sh. mil. 10
 Sehemu ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Dodoma mjini
 Baadhi ya wazee Mkoa wa Dodoma wakiwa katika mkutano huo
 Komredi Kinana akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini kwa kutoa taarifa nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
 Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa msingi wa Ofisi ya CCM Tawi la Bahi Road
 Kinana akishiriki ujenzi wa chumba cha darasa katika Shule ya Sekondari Lukundo mjini Dodoma leo
 Kikundi cha ngoma za utamaduni wa Kigogo, cha Nuru, kikitumbuiza wakati Komredi Kinana alipowasili Kata ya Nzuguni kushiriki ujenzi wa mradi wa maji.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Luteni Chiku Galawa, akishiriki kuchimba mtaro wa mradi wa maji katika Kata ya Nzuguni
 Komredi Kinana akishiriki katika ujenzi wa mradi wa maji katika Kata ya Nzuguni, Jimbo la Dodoma Mjini
 Kikundi cha ngoma cha Hiari ya Moyo kikitumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Barafru, mjini Dodoma leo
 Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa katika mkutano huo wa hadhara
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma

 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Dodoma, ambapo ametoa ushauri kwa Katibu Mkuu Kiongozi, kuwasimamisha mara moja watumishi wanaotajwa kwenye sakata la Escrow  kama CCM ILIVYOWASIMAMISHA VIONGOZI WATATU waliotajwa kwenye sakata hilo
 Kinana akimpongeza Bianka Mass wa chama cha Chadema aliyetangaza kujiunga na CCM katika mkutano huo. Zaidi ya wanachama 1000 walijiunga na chama hicho.
 Komredi Kinana akiongoza kula kiapo cha CCM wakati wa mkutano huo
 Baadhi ya akina mama waliojunga na CCM wakila kiapo  cha chama hicho wakati wa mkutano huo
Komredi Kinana akijadiliana jambo na Job Lusinde mmoja wa wazee walioitumikia Serikali na chama kwa uaminifu mkubwa baada ya mkutano huo kumalizika

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.