MWANAHARAKATI WA SIKU NYINGI WA WANYAMAPORI NCHINI TANZANIA AMPONGEZA RAIS KENYATTA

      

IMG_1715
Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini Tanzania Kidon Mkuu, akiwa Philipine Manila December 2014 kwenye harakati zake za matatembezi ya kupinga kuuwawa kwa Tembo na Faru akiwa na wanaharakati wenzake wa huko Philipine
IMG_1734
Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini Kidon Mkuu, akiwa Philipine Manila December 2014 kwenye matatembezi ya kupinga kuuwawa kwa Tembo na Faru akiwa na Susan Jaylo
IMG_1693
Mwanaharakati Kidon Mkuu akiwa kweye hoteli alikoshukia ya Sofitel mjini Manila Philipine
…………………………………………………………………….
Na Pamela Mollel,Arusha
Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini Tanzania Bw.Kidon Mkuu amempongeza Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa kitendo cha kuchoma moto meno ya tembo tani 15 katika kuhadhimisha siku ya wanyamapori Dunia
Bw.Mkuu aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati akiongea na vyomba vya habari kuhusu siku ya wanyamapori dunia, ambapo alisema kuwa anamuunga mkono Rais huyo kwa kufanya tukio hilo la kihistoria la kuchoma meno ya tembo
Alisema faida ya kufanya hivyo ni kudhibiti masoko na mianya ya kusafirisha meno hayo hali itakayosaidia ujangili wa tembo kupungua
Aidha alitoa wito kwa serikali na wizara kuhamasisha jamii kuhusu siku ya wanyamapori dunia kama wanavyofanya nchi zingine hali itakayosaidia jamii kufahamu wajibu wao wa kulinda wanyamapori
Siku ya Wanyamapori Duniani ilitangazwa na Baraza la Umoja wa Mataifa Desemba 20, 2013 ili kuhamasisha kulinda wanyamapori na mapori na uhadhimishwa tarehe3 April kila mwaka

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.