TASAF YAWAFUNDA WAANDISHI WA HABARI WA MIKOA YA LINDI NA MTWARA


 Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili waweze  kutumia vyombo vya habari vilivyoko kwenye maeneo yao kutangaza habari za Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa naMfuko huo.

Akifungua mafunzo hayo yanayoendeshwa kwa utaratibu wa Kikao Kazi Mkurugenzi Mtendajiwa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema kazi ya kutokomeza umaskini nchini inahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari.

Bwana Mwamanga amesema tangu TASAF ianze kutekeleza Mpango wa kunusuru kaya masikini kumekuwa na mafanikio makubwa hususani katika maeneo ya walengwa ambao wameanza kuboresha maisha yao na katika baadhi ya maeneo walengwa wameanza kukuza shughuli za kiuchumi huku wengine wakiweza kuhudumia kaya zaokinyume na hali ilivyokuwa huko nyuma.

Amewasihi waandishi wa habari kuwatembelea walengwa wa Mpango huo ili kuona namna walengwa hao wanavyonufaika na Mpango huo wa uhawilishaji fedha na kisha kutangaza mafanikio yaliyokwisha patikana huku akisisitiza kuwa hata pale penye changamoto zionyeshwe ili marekebisho yafanyike kwa manufaa ya walengwa
Zifuatazo ni baadhi ya picha za washiriki wa kikao kazi hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo kikuu Huria Mjini Mtwara.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bwana RenatusMongogwela (mwenye shati nyeupe)akizungumza na ujumbe wa TASAF ulioongozwa na Mkurugenzi mtendaji Ladislaus Mwamangawa, kwanza kushoto kwa kaimu katibu tawala.
  Mkurugenzi Mtendajiwa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga aliyesimama akifungua kikao kazi cha watendajiwa TASAF kutoka maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini na waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi (hawapopichani) 
 Washiriki wa kikao kazi cha watendaji wa TASAF  na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga(hayupo pichani).
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana  Ladislaus Mwamanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF makao makuu baada ya kufungua kikao kazi cha waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi.
 Mkurugenzi Mtendajiwa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF makao makuu baada ya kufungua kikao kazi cha waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.