BONANZA LA TAASISI 15 LAFANA ARUSHA

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Adollah Mapunda akikagua timu ya netiboli wakati wa Bonanza lililoshirikisha taasisi 15 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Wachezaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), wakifurahia zawadi ya kuku waliyotwaa baada ya kuibuka kidedea katika mashindano ya kukimbiza kuku wakati wa Bonanza lililoshirikisha taasisi 15 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha


Richard Mwangulube

Timu ya Soka  ya chuo cha ufundi Arusha (ATC) imefnikiwa kubeba kombe  la bonanza  baada ya kuilipua timu ya soka ya Benki Kuu Tawi la Arusha ( BOT mabao 3-0

Ushindi huo wa  timu ya ATC umekuwa faraja kubwa kwa  chuo hicho kutokana na mashindano hayo yaliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa mara ya kwanza

Katika bonanza hilo timu ya soka ya Mamlaka ya Maji Arusha (AUWSA)  ilishika  nafasi ya pili

Kwa upande wa netiboli timu ya RAS  Arusha  ilipata ushindi mnono baada ya  kuwaadhibu ndugu zao timu ya Jiji la Arusha katika mchezo wa fainali

Katika mchezo wa  draft ATC wanaume  imeibuka kidedea tena huku  timu ya  chuo cha uhasibu tawi la arusha ikishika nafasi ya pili

Kwa upande wa wanawake  Halmashauri ya Arusha (Arusha DC)  imefanikiwa kuinyuka  timu ya chuo cha uhasibu

Kuhusu mchezo wa  bao timu yaMamlaka ya Maji Arusha iliibuka na ushindi baada ya kuwacharaja vijana wa  kituo cha mikutano cha kimataifa AICC kwa upande wa wanaume

Katika mchezo w akarata  uhasibu wamepata ushindi  huku nafasi ya pili  ikichukuliwa na AICC upande wa wanaume

Katika mchezo huo wanawake  Jiji Arusha wameshika nafasi ya kwanza  ikifuatiwa na RAS Arusha

Katika kuvuta kamba wanaume  chuo cha uhasibu Arusha kimeshika nafasi ya kwanza  huku mshindi wa pili ikichukuliw ana  chuo cha ufundi Arusha upande wa wanaume

Kwa upande wa wanawake  kuvuta kamba  Timu ya Jiji Arusha  imefanikiw akunyakua nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikichukuliw ana  Ras Arusha

Katika mchezo wa kukimbia  na magunia wanaume taasisi ya utafiti TAWIRI ilishika nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikinyakuliw ana AICC

Upande wa wanawake kukimbia na magunia  Uhasibu nafasi ya kwanza  huku nafasi ya pili ikichukuliw ana TAWIRI

Kuhusu mbio za  watu wazima  wenye umri  zaidi ya miaka 50 Ofisi ya RAS ilishika nafasi ya kwanza  ikifuatiwa na AICC upande  wa  wanaume

Upande wa wanawake  nafasi ya kwanza ilichukuliwa na TPRI huku nafasi ya pili ikichukuliwa na RAS ili kufanikisha bonanza hilo la kwanza  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felex Ntibenda aliunda timu ya watu 18 kutoka taasisi mbalimbali

Bonanza  la mwaka huku  ambalo ni la kwanza taasisi zipatazo 15   zimeshikiriki  katika mashindano mbalimbali  ukiwemo mchezo wa kufukuza kuku

Aidha washindi wa kwanza na  wa pili walizawadiwa vikombe na medali pamoja na  wengine kubahatika kupata zawadi ya kuku na vyeti
 Bonanza hilo lilifanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.