Balozi
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, ambaye ni Mwanamitindo
na Mbunifu Mavazi maarufu nchini Tanzania, kwa sasa akifanyia kazi zake
nchini Marekani, akizungumza wakati wa semina ya siku moja, iliyowaleta
pamoja, wanamitindo "kinda" wa Tanzania, kwenye hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam Jumapili Mei 17, 2015.
Semina hiyo ililenga kuwafunza na
kubadilishana uzoefu juu ya tasnia hiyo inayokuwa kwa kasi. Semina hiyo
ya siku moja, ilitayarishwa kwa pamoja na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na
mwanamitindo huyo nguli. Katika maelezo yake, Flaviana, alisema yeye
binafsi ni mwanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa hiari yaani "PSPF
Supplementary Scheme-kwa kifupi PSS", na kuwataka wanamitindo
waliohudhuria semina hiyo, kufuata nyayo zake.
Aliwaeleza umuhimu wa
wanamitindo hao ambao wengi ni vijana, kujiunga na mpango huo kwa faida
yao ya sasa na baadaye, kwani yeye anafaidika sana kuwa mwanachama wa
Mfuko huo. Baada ya maelezo hayo yaliyofuatiwa na balozi mwingine wa
Mfuko huo, Msanii maarufu wa muziki wa majigambo, Mrisho Mpoto, naye
aliwapa "doze" wanamitindo hao juu ya ukuhimu wa wao kuchangamkia fursa
mapema kwani ndio mtindo wa kisasa.
Hali kadhalika afisa masoko wa Mfuko
huo Magira Werema, aliwahakikishia wanamitindo hao kuwa Mfuko huo ni
Mfuko bora na wala hawatajuta waingiapo kuwa wanachama. Baada ya hotuba
hizo, wanamitindo hao walizichangamkia fomu za kujiunga na uanachama wa
Mfuko huo amba;po karibu washiriki wote zaidi ya 100 walijiunga na Mfuko
huo.
Wanamitindo
wakiwa kwenye foleni ya kupiga picha tayari kujipatia vitambulisho
baada ya kukamilisha zoezi la kujaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS
wa Mfuko huo.
Wanamitindo wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS.
Afisa
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Magira Werema, akitoa maelezo ya
kina kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na Mfuko huo.
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akizungumza jambo
na wenzake, Magira Werema, (kushoto), na Colleta Mnyamani, ambaye ni
Afisa Uhusiano wa Mfuko huo.
Flaviana
(kulia) na Zuli Remtula,(katikati), mwanamitindo mwingine nguli
nzhini,na washiriki wengine wa semina hiyo, wakifuatilia maelezo
yaliyokuwa yakitolewa na Afisa wa PSPF, Magira Werema.
Comments