MAWAZIRI WA NISHATI WAJADILI KUHUSU NISHATI ENDELEVU KWA WOTE

Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa Mawaziri kuhusu nishati, mkutano ambao ulifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson siku ya Jumatano.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Charles Kitwanga akiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, unapofanyika mkutano wa Mawaziri wa Nishati kutoka mataifa mbalimbali duniani, mkutano ambao pia unawashirikisha wadau na wataalamu wanaohusika sekta ya nishati.

Na Mwandishi Maalum, New York
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe.Charles Kitwanga ( Mb), ni miongoni mwa mawaziri kutoka mataifa mbalimbali duniani wanaohudhuria mkutano wa kila mwaka kuhusu Nishati Endelevu kwa Wote (SE4All)

Mkutano huu unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, ambao siku ya jumatano mawaziri wameanza kujadili na kubadilisha uzefu kuhusu eneo hilo la nishati ambalo linaelezwa kuwa ni muhimu kwa maendeleo endelevu kijamii, kiuchumi na mazingira .

Mhe. Kitwanga ambaye anatarajiwa kuelezea msimamo wa Tanzania katika eneo hili la nishati endelevu siku ya alhamisi ( leo). Ameambatana na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ngosi Mwihava pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

Akifungua mkutano wa Mawaziri, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson, amesema mkutano huo wa mawaziri na ambao ulitanguliwa na mijadala mbalimbali iliyofanyika nje na Makao Makuu, kuwa Mawaziri hao wanakutana katika wakati muafaka na hasa kwa kuzingatia kwamba mwaka huu wa 2015 ni muhimu sana kwa Umoja wa Mataifa na Nchi wanachama.

Akasema , viongozi wa dunia wametambua kwamba, njia sahihi ya kufikia mafanikio ya pamoja sasa na baadaye ni kuwa na uwiano uliosawa kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Naibu Katibu Mkuu, ameongeza kuwa kwa muda mrefu, jumuiya ya kimataifa imekuwa ikifuata njia za ukuaji wa pamoja pasipo kuheshimu mipaka baina ya mazingira ya dunia na haja ya kuishi kwa kuzingatia uwiano bora na viumbe wengine.

Na kwa sababu hiyo, Bw. Jan Eliasson amewaeleza Mawaziri hao na wadau wengine wanaoshiriki mkutano huu kuwa, mwaka huu Jumuiya ya Kimataifa itakuwa na mikutano mitatu muhimu na ambayo itatoa mwelekeo mpya na ajenda mpya kuhusu maendeleo endelevu kwa wote.

Ameitaja mkutano hiyo mitatu na muhimu kuwa ni , Mkutano utakaofanyika mwezi Julai Addis Ababa, Ethiopia, mkutano ambao dhumuni lake kuu litakuwa ni kujadili na kukubaliana kuhusu mfumo wa fedha kwaajili ya utekelezaji wa maendeleo endelevu.

Mkutano wa pili ambao ameutaja ni ule utakofanyika mwezi Septemba hapa New York, mkutano ambao Wakuu wa Nchi na Serikali watapitisha ajenda na malengo ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015.

Aidha mkutano wa tatu ni ule utakaofanyika Jijini Paris, Ufaransa mwezi Desemba, ambapo makubaliano yanatarajiwa kufikia kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi.

Akizungumzia kuhusu nishati endelevu, Naibu Katibu Mkuu, ameeleza kwamba Nishati endelevu ndio msingi mkuu wa maendeleo na mageuzi katika sekta zote ziwe za viwanda, kilimo au ustawi wa jamiii na kuongeza kuwa katika dunia ya sasa ambayo inakabiliwa na changamoto nyingi, ufumbuzi wa changamoto hizo unahitaji ushirikiano wa pamoja baina ya serikali, sekta binfasi na makundi mengine ya kijamii

Akasisitiza kuwa mpango kuhusu nishati endelevu kwa wote, umeonyesha kwamba ushirikiano miongoni wa wadau mbalimbali umeweza kusaidia kusukuma mbele ajenda hiyo ya nishati endelevu kwa wote.

Ameongeza kuwa kizazi kijacho kitakichangaa kizazi cha sasa kwa kutoweka mipango madhubuti kwaajili yao.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Taifa akabainisha pia kwamba, Nchi zaidi ya 80 zinazoendelea zimejiunga mpango huo wa nishati endelevu kwa wote. Na kwamba Ahadi zenye thamani ya mabilioni ya dola tayari zimepatikana.

Ripoti kuhusu kuhusu mchakato wa kuelekea nishati endelevu ambayo ilitolewa kwa washiriki wa mkutano huo Mei 18, inaonyesha kwamba watu 1.1 bilioni duniani kote wanaishi bila nishati ya umeme. Huku karibu wengine 3 bilioni wakiendelea kupika kwa kutumia nishati ambazo si salama kwao na mazingira, nishati hizo ni pamoja na mkaa, kuni, mafuta ya taa na sam

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.