UNESCO YASISITIZA UPENDO KWA WATOTO WENYE ALBINISM

DSC_0945Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akiambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir (kushoto) walipotembelea shule msingi Mitindo ya watoto wenye ulemavu wa ngozi, macho na masikio iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza. Kulia ni Mtaalamu wa Jinsia na Haki za Binadamu kutoka UNESCO Tanzania, Bi. Annica Moore.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
………………………………………………………..
Na Modewjiblog team
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)Tanzania, Zulmira Rodrigues amesisitiza umuhimu wa kuwapenda watoto wenye ulemavu wa ngozi katika jamii baadala ya kuwatenga .
Zulmira alisema hayo alipotembelea watoto wenye ulemavu wa ngozi katika shule ya msingi ya Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza mwishoni mwa juma
Shule hiyo ya serikali ina wanafunzi zaidi ya 1000 wakimo wenye ulemavu 202 .
Kati yao 81 ni wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ambao wanahifadhiwa na serikali katika shule hiyo maasa 24 kufuatia wimbi la mauaji la watu wenye ulemavu wa ngozi katika mikoa ya kanda ya ziwa .
Hata hivyo Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO Tanzania alionekana kupatwa huzuni kubwa kutokana hali ya maisha ya watoto hao .
“ Nimehuzunika sana (I am so sad). Sio tabia ya watu wa Afrika kuwatenga watu wanyonge (weak people)”alisema huku akitokwa na machozi mara baada ya kuwatembelea watoto hao na kuongea nao pamoja na uongozi wa shule hiyo.
Alisema ni muhimu watoto hao wenye ulemavu wa ngozi kuwa wanavaa nguo za mikono mirefu ili kuwakinga na jua kwa ajili ya kulinda afya zao.
Hata hivyo Zulmira alipongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi na kutoa wito kwa wadau wote kuunga mkono juhudi hizo.
DSC_0955Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mwalimu msingi Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Katika ziara hiyo, Zulmira alikuwa amefuatana na mbunge wa viti maalum anayewakilisha watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) Mh. Al shaymaa Kwegyir.
Mbunge huyo pia alisema kitendo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi kukosa malezi na mapenzi ya wazazi ni changomoto kubwa iliyopo kwa sasa.
Alisema ni jukumu la watu wote kulinda na kusadia kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
“Ufumbuzi wa matatizo ya wetu wenye ulemavu wa ngozi sio kazi ya serikali tu, ni jukumu la kila mtu”,mbunge huyo alisisitiza.
Aliahidi kuwasilisha bungeni baadhi ya changamoto zinazowakabili wanafunzi walemavu waliopo katika shule hiyo ya Mitindo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Kurwa Ng’hwelo alisema serikali inatumia zaidi ya shilingi milioni 10 kuwa ajili ya mahitaji ya chakula kwa wanafunzi wote wenye ulemavu wapatao 202 kila mwezi.
Shule hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wanaosadia wanafunzi hao walemavu.
DSC_0968Mwalimu wa shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng’hwelo akitoa maelezo ya idadi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma shuleni hapo ambao ni 202 huku 81 wakiwa na albinism kwa Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kushoto) aliyetembelea shule hiyo kuangali changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu wa ngozi.
DSC_0979Mwalimu wa shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng’hwelo akimwonyesha mazingira ya eneo la shule hiyo Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues aliyeambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir.
DSC_0989Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa kutwa wanaosoma katika shule ya msingi Mitindo mara baada ya kuwasili shuleni hapo akiwa ameambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir.
DSC_0993Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza na wanafunzi hao waliofurahia ujio wake.

DSC_0997Pichani ni moja ya jengo lililojengwa na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania.
DSC_1009Mmoja wa watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) akitoka bwenini kuelekea chumba maalum kwa ajili ya kujipatia chakula cha mchana katika shule ya msingi Mitindo huku akionekana kutembea kwenye jua kali pasipo na kuwa na nguo ndefu ya kufunika hadi mikononi kujikinga na mionzi ya jua inayopelekea kupata saratani ya ngozi.
DSC_1017Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albinism) ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akila chakula cha machana huku akijikuna kutokana na maumivu makali anayosikia ya majeraha ya mionzi ya jua iliyoharibu mikono yake na kubadilika rangi ambayo athari yake baadae ni saratani ya ngozi.
DSC_1025Na hii ndio hali halisi ya binti huyu katika mikono yake kutokana na kutembea kwenye jua bila kusitiri mikono yake na nguo ndefu.
DSC_1026Baadhi ya watoto wa bweni wenye Albinism wakijipatia chakula cha mchana jikoni.
DSC_1043Mtoto mwingine aliyeathiriwa na mionzi ya jua miguuni na kupelekea kubadilika rangi kuwa mwekundu kutokana na kukosa nguo ndefu za kujisitiri na mionzi ya jua… wakiendelea kujinoma na chakula cha mchana.
DSC_1033Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akionyesha uso wenye huzuni kubwa kutokana na mazingira magumu waliyonayo watoto hao shuleni hapo. Kushoto ni Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir aliyeambatana na Bi. Zulmira Rodrigues kutembelea shule hiyo. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng’hwelo.
DSC_1068Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Mitindo, Kalunde Cosmas alipofanya ziara fupi ya kutembelea shule hiyo na kujionea changamoto zinazowakibili watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albinism).
DSC_1036Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akimwonyesha mwandishi wa modewji blog (hayupo pichani) majeraha ya kuungua na jua kwa mmoja wa watoto mwenye albinism shuleni hapo.
DSC_1053Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aliyekuwa akijipatia chakula cha mchana.
DSC_1073Mdau Semeni Kingaru akimsimamia kula chakula cha mchana mtoto mdogo kuliko wote mwenye albinism aliyeonekana kukosa upendo wa wazazi wake kwa kipindi kirefu na kufarijiwa na ugeni huo uliofika shuleni hapo.
DSC_1101Mbunge wa viti maalum CCM,anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akibadilishana mawazo na mabinti wa shule ya msingi Mitindo alipowatembelea na Bi. Zulmira Rodrigues.
DSC_1106Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akisaidiana na Mdau Semeni Kingaru kugawa zawadi ya juisi kwa watoto wa shule ya msingi Mitindo.
DSC_1113Mtaalamu wa Jinsia na Haki za Binadamu kutoka UNESCO, Bi. Annica Moore aliyeambatana na Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (hayupo pichani) akifurahi jambo wakati akigawa zawadi ya juisi mmoja watoto wenye albinism shuleni hapo.
DSC_1119Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiendelea na zoezi la ugwaji zawadi ya juisi kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi, macho na masikio wa shule ya msingi Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza alipowatembelea mwishoni mwa juma akiwa ameambata na Mbunge wa viti maalum CCM,anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir (hayupo pichani).
DSC_1085Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa macho wakijumuika na wenzao wenye ulemavu wa ngozi na masikio kujipatia chakula cha mchana.
DSC_1087Mtoto mdogo kuliko wote mwenye albinism anayeonekana kukosa lishe bora inayostahili kutokana na umri wake ambapo modewjiblog imebaini kuwa mtoto huyu ana “Utapiamlo” kutokana na kukosa lishe hiyo bora. Dalili moja wapo ni tumbo lake kuwa kubwa na gumu.
DSC_1137Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimnywesha juisi mtoto mdogo kuliko wote anayelelewa kwenye shule ya msingi Mitindo ya watoto wenye uhitaji maalum ambao ni walemavu wa ngozi, macho na masikio alipofanyia ziara fupi mwishoni mwa juma mkoani Mwanza.
DSC_1144Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimnyeshwa juisi mtoto menye ulemavu wa macho alipotembelea shule ya msingi Mitindo iliyopo wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza.
DSC_1160Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwa na uso wa huzuni kutokana na mazingira ya watoto hao na kupelekea kumwaga machozi kwa uchungu yeye kama mama mwenye kuthamini upendo. Kushoto ni Mh. Al Shaymaa Kwegyir.
DSC_1163Bw. Abdulaziz Mbegele wa kitengo cha Logistic kutoka UNESCO, akimnywesha juisi mtoto mwenye ulemavu wa macho wakati wa ziara hiyo na Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania.
DSC_1091Mtoto alyefahamika kwa jina moja tu Kevin mwenye umri wa miaka 11 ambaye alifikishwa kwenye shule hiyo akiwa mdogo sana na wazazi wake kumtelekeza hadi leo huku akiwa hamjui mama, baba, mjomba, dada, kaka wala shangazi….. kisa amezaliwa na albinism….!
DSC_1097Mtoto Kevin akipata “self” na mjomba wake mpya Zainul Mzige wa modewjiblog aliyeambatana na ugeni huo.
DSC_1202Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza na waandishi wa habari na kutoa hisia zake kuhusiana na changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu wa nguvu na kusisitiza upendo kwa watu wenye albinism.
DSC_1216Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Serikali yajipanga kuboresha mazingira rafiki ya hedhi Salama kwa wanafunzi

unnamed
Mratibu wa huduma ya Maji, Afya na Usafi wa mazingira shuleni kutoka wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi Theresia Kuiwite (Katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Hedhi Duniani yatakayofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania tarehe 28 Mei, yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mwaka huu Ikiwa “Usisite Kuzungumzia Hedhi”. Wengine kushoto ni Mwandaaji wa maadhimisho hayo kutoka kampuni ya Kasole Secrets LTD, Bi. Hyasintha Ntuyeko na Bi Emmy Manyelezi (Kulia) ambae ni Mratibu wa mradi kutoka shirika la Water Aid Tanzania.
…………………………………………………
Na Mwandishi Wetu,
SERIKALI imetangaza programu maalumu inayolenga kuziwezesha shule za msingi na sekondari hapa nchini kuwa na vyumba maalumu tofauti na choo vitakavyo wawezesha wanafunzi wa kike kupata faragha za usafi wakati wa hedhi wakiwa shuleni.
Hatua hiyo ya serikali iliwekwa bayana na Mratibu wa huduma ya Maji, Afya na Usafi wa mazingira shuleni kutoka wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi Theresia Kuiwite alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku hedhi duniani yanayotarajiwa kuadhimishwa Mei 28 mwaka huu.
“Lengo ni kupunguza tatizo la mahudhirio hafifu miongoni mwa wanafunzi wa kike ambao wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa kwenye hedhi kutokana na ukosefu wa miundombinu rafiki inayoweza kuwapa faragha za wao kufanya usafi wanapokuwa kwenye hali hiyo,’’ alisema.
Kwa mujibu wa Bi. Kuiwite, mpango huo tayari umekwishaanza kutekelezwa katika baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwemo wilaya ya Njombe huku akibainisha kuwa kwa sasa wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo yao kwa zaidi ya siku 3 hadi 5 kutokana na hedhi jambo linalozorotesha ufahulu wao darasani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kasole Secrets LTD, Bi. Hyasintha Ntuyeko ambae pia ni mdau na muandaaji wa  maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani  alisema Kampuni yake kwa kushirikiana na wadau wengine wameamua kuitumia siku hiyo kuhamasisha mabadiliko ndani ya jamii hususani mila na desturi zinazosababisha suala la hedhi kwa mwanamke lionekane kama ni jambo la aibu kwa jamii.
“Ukweli upo wazi kwamba hata matatizo mengi ya wanawake kuhusiana na uzazi chimbuko lake ni kushindwa kwao kukabiliana na hedhi kwa njia salama haswa walipokuwa katika umri mdogo. Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni ‘USISITE KUZUNGUMZIA HEDHI’“, alibainisha.
Kwa mujibu wa Bi. Hyasintha, maadhimisho hayo yataongozwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Anna Kilango Malecela na yanatarajiwa kupambwa na matembezi ya hiari yatakayoanzia Wizara ya elimu saa 34:00 asubuhi – 06:00 mchana na kumalizikia katika viwanja vya Mnazi Mmoja siku ya tarehe 28,Mei, 2015.
Naye Bi Emmy Manyelezi ambae ni Mratibu wa mradi kutoka shirika la Water Aid Tanzania alitoa wito kwa wadau mbalimbali hususani sekta binafsi kuhakikisha wanaisaidia serikali katika kuhakikisha kuwa vifaa muhimu vinavyohusu masuala ya hedhi zikiwemo pedi za wanawake vinawafikia wananchi wote hususani waliopo vijijini na kwa bei nafuu.
Zaidi ilielezwa kuwa maadhimisho hayo pia yatatoa fursa kwa washiriki kubadilishana elimu juu ya usafi wa hedhi, uzoefu, changamoto na ufumbuzi endelevu kwa ajili ya wasichana wa mashuleni na wanawake kwa ujumla.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.