Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari
JESHI la
Polisi mkoani Katavi linawashikilia watu tisa wakiwemo vikongwe wa miaka
80 na 70 baada ya kukamatwa wakiwa na bunduki tatu za kienyeji aina
magobole, risasi zake 15, mtambo wa kutengenezea silaha, baruti na sare
za Jeshi la Wananchi la Ulinzi na Usalama (JWTZ).
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari alitaja vitu vingine
vilivyokamatwa kufuatia msako mkali unaoendelea wilayani Mlele ni
vipande tisa vya nondo, vyuma vya kutengenezea risasi na mafuta ya
kiboko yaliyohifadhiwa kwenye chupa.
"Mafanikio
haya yametokana na ushirikiano mzuri kati Jeshi la Polisi, askari wa
Tanapa na raia wema ambapo wamekuwa wakiendelea kutoa taarifa za uhalifu
na wahalifu na kufanikisha katika ukamataji," alieleza .
Alidai
kuwa silaha hizo zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria na zilikuwa
zikitumika katika visa vya kijangili na uhalifu mwingine wilayani Mlele.
Akizungumza
kwa njia ya simu, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Lazaro
Zakaria (63) aliyekamatwa akimiliki gobole bila kuwa na kibali, Shaaban
Mussa (52) gobole bila kuwa na kibali na Robert Kaumba (80).
Wengine
ni Hamisi Rehani (70) alikamatwa akiwa na mtambo wa kutengenezea silaha
aina ya gobole bila kuwa na kibali, Benedict Simon (52) akiwa na risasi
15 za gobole, vipande tisa vya nondo, vipande vya miti, mtutu mmoja na
baruti ndani ya chupa na Shaaban Mussa (52) alikamatwa akiwa na risasi
moja ya gobole bila kibali.
Kwa
mujibu wa Kidavashari, katika msako huo pia jeshi hilo lilimtia mbaroni
Esther John (21) akiwa na sare ya JWTZ na vyuma viwili vya kutengenezea
risasi na Mashaka George (32), alikamatwa akiwa na mafuta ya kiboko
aliyoyahifadhi kwenye chupa.
Alieleza
kuwa watuhumiwa wote, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa upelelezi na
watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.CHANZO: HABARI LEO (Muro)
Comments