Biashara, usafiri na idadi ya watu mjini Nairobi imepungua kwa kiasi kikubwa saa chache kabla ya kuwasili kwa rais Obama
Abiria na madereva wanaotumia Bbararabara kuu jijini Nairobi wameathirika pakubwa na mipango kabambe za usalama zilizowekwa kwaajili ya ujio wa rais huyo wa Marekani.
Mabarabara yanayokaribiana na ile itakayotumika na Obama zimefungwa kwa umma.
Na si hayo tu njia zote mkabala na zile zitakazotumika pia zimefungwa.
Obama anatarajiwa kutua nchini Kenya wakati wowote kutoka saa moja
Sekta ya matatu, njia kuu ya usafiri imelemazwa huku wahudumu wa magari ya abiria wakieleza kutokuwa na wateja.
Raia wengi wanaotumia barabara za Uhuru an Mombasa waliondoka mjini mapema huku wakihofia kuathirika na hatua ya kufungwa kwa barabara wanazotumia.
Maduka mengi ya kibiashara pia yalifungwa huku wafanyibiashara wakieleza kuandikisha idadi ndogo au hata kutoweko kwa wateja.
Comments