SILAHA ZILIZOPORWA NA MAJAMBAZI KITUO CHA POLISI STAKISHARI ZANASWA

 Baadhi ya silaha zilizoporwa na majambazi walivamia Kituo cha Polisi cha Stakishari Ukonga, na kuua polisi wanne na raia watatu zikioneshwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam baada ya  kuzikamata katika msako mkubwa na kuzikuta zikiwa zimefukiwa chini wilayani Mkuranga, Pwani, ambapo pia walikuta kwenye sanduku la chuma sh. mil. 170.

Majambazi watano wamekamatwa na wengine watatu walikufa walipokuwa wakikimbizwa Hospitali baada ya kujeruhiwa katika mapambano makali na polisi. Jumla ya silaha 16 zilikamatwa zikiwemo 14 zilizoporwa Stakishari. (PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA)

Pia baada ya kufukua kwenye shimo katikati ya msitu/vichaka katika Kijiji cha Mandimkongo, Kata ya Bupu, wilayani Mkuranga,walikuta sanduku la chuma likiwa na sh. mil. 170 noti za elfu kumi na elfu tano.

Majambazi waliokufa ni Abbas Hashim, Mkazi wa Mbagala, Yasin Mkazi wa Kitunda Kivule na Said Mkazi wa Kitunda Kivule.


 Fedha sh. mil 170 zilivyokuwa zimepangwa kwenye sanduku la chuma na kufukiwa chini
 Baadhi ya pikipiki zlizotumiwa na majambazi walipovamia kituo cha polisi cha Stakishari
 Picha za majambazi wanaoendelea kutafutwa
Pikipiki zilizotumika katika tukio la iujambazi katika Kituo cha Polisi Stakishari

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.