Unaikumbuka Hii.....Barua ya Mfungwa Papii Kocha kwa Rais JK.



BARUA YA PAPII KOCHA
KWA RAIS
JAKAYA KIKWETE... KWA
WALE
AMBAO HAMJAISOMA HÍI
HAPA.
MF/NA: 836'04
Johnson Nguza
(Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam
Mh. Rais Jamuhuri ya
Muungano
Tanzania
YAH: MAOMBI YA
KUPEWA MSAADA
(MSAMAHA) WA
KUFUTIWA ADHABU
YA KIFUNGO NILIYOPEWA
NA
MAHAKAMA YA HAKIMU
MKAZI
KISUTU.
Husika na somo hilo hapo
juu.
Mimi ni mfungwa katika
gereza
kuu Ukonga. Kwa heshma
na
taadhima na kwa
kutambua utu
na huruma yako ya
kiMUNGU
ulionayo dhidi ya
binadamu
wenzako pamoja na
mamlaka
uliokabidhiwa na Jamuhuri
ya
Muungano wa Tanzania.
Naanguka na kushika
miguu yako
mitukufu muheshimiwa
rais.
Nakuomba msaada
(msamaha)
kwako muheshimiwa
rais, kwa
njia hii ya maandishi
kusudi
niweze kuondolewa
adhabu ya
kifungo cha maisha
gerezani,niliyohukumiwa
na
mahakama tajwa hapo
juu.
Mh.Rais mimi
nimefungwa nikiwa
bado kijana mwenye umri
mdogo,
na ukweli kutoka moyoni
sikufanya kosa hilo. Si
mimi, baba
yangu Nguza wala ndugu
yangu
yeyote aliyefanya
kitendo kile.
Lakini wenye mamlaka
wakatuona tuna hatia na
kuamua
kuteketeza kizazi chetu
gerezani.
Natamani kiama ifike ili
mwenyezi
Mungu aweke wazi
ukweli wote
uliojificha nyuma ya pazia.
Mpaka
sasa natambua wazi
hatima
pamoja na dhamana ya
maisha
yangu ipo katika mikono
yako
mitukufu Mh. Rais
Naomba huruma yako
muheshimiwa Rais
maana mimi ni
mtoto wako ninaehitaji
huruma
yako wewe mzazi. Lakini
pia sisi
ni binadamu wenye nafsi
na miili
kama wengine.
Waliotumia mamlaka yao
kutuweka gerezani nao ni
binadamu pia, wenye miili
na
nafsi. Ipo siku nafsi zetu
zitapaswa kutoa hesabu
ya
tuliyoyafanya hapa
duniani.
wakati huo miili yetu
tunayoitumia
kunyanyasa
wanyonge itakuwa
imeoza
mavumbini.
Natumaini kauli yako ya
mwisho
ndio itakayoleta pumzi ya
uhai
nafsini mwangu.
Nakutakia kazi
njema, afya njema na
maisha
marefu.
Mungu akubariki.
Wako mtiifu
Mfungwa NO:836'04
JOHNSON
NGUZA (PAPII KOCHA)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.