WANASAYANSI ZAIDI YA 2000 WASHIRIKI MKUTANO WA TABIANCHI, PARIS UFARANSA

Royal CfCC15.jpgwPichani: Baadhi ya Wanasayansi wakifuatilia mawasilisho ya wanasayansi wenzao yaliyokuwa yakiwasilishwa katika mkutani huo ulioanza Julai 7 na kumalizika Julai 10, mwaka huu katika ukumbi mkubwa wa makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa.
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[Paris, Ufaransa] Wanasayansi zaidi ya 2500, kutoka pembe zote duniani wamekutana katika mkutano mkubwa wa wanayasansi juu ya siku za usoni na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ‘Our Common Future Under Climate Change’. 
Mkutano huo ulioandaliwa katika makao makuu ya UNESCO mjini Paris, Ufaransa, ulikuwa wa siku nne (Julai 7-10) na ndio ulikuwa mkutano mkubwa zaidi wa wanasayansi duniani kuanda makataba ambao unatarajiwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi utakaofanywa hapo Desemba, mjini Paris.
Ushiriki wa wanasayansi hao katika mkutano wao huo umefanya jiji la Paris kuwa na pilikapilika za hapa na pale hasa viunga vya makao makuu ya UNESCO na yalipokuwa yanafanyika matukio ya mkutano huo.
Miongoni mwa mada zilizowakilishwa katika mkutano huo ni pamoja na namna ya dunia itakavyokabiliana na kiwango cha hali ya joto na nyuzi mbili (to reduce temperature level by 2 degrees), mafuliko yanayokumba nchi mbalimbali duniani (Floods). Mada zingine ni kama vile misitu, athari za watu kuongezeka mijini, ongezeko la joto, kupungua kwa vina vya bahari, masuala ya hewa ukaa, gesi sumu na mengine mengi yanayopelekea athari za tabianchi.
Mkutano huu ulilenga jinsi ya kukabiliana na tabianchi pamoja na kubadilishana ujuzi zaidi hii ikiwa ni kuelekea mkutano mkuu wa 21 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiriko ya Nchi (COP21) utakaofanyika hapa hapa Paris , Desemba mwaka huu.
Hata hivyo matarajio ya wanasayansi wengi wakiwemo kutoka nchi tofauti wameeleza kuwa, hadi kufikia mkutano wa COP 21, hiyo Desemba mataifa yataafikiana maamuzi ya kila mmoja wapo pindi watakapo wasilisha.
18898203484_c8cbf79953_kBaadhi ya wanasayansi wakiendelea na mkutano katika moja ya kumbi za mikutano katika viunga vya Makao makuu ya UNESCO, Paris Ufaransa.

19334259259_2b251d5d24_oBaadhi ya wanahabari wakifanya mahojiano na mmoja wa wanasayansi katika mkutano huo katika viunga vya Makao makuu ya UNESCO, Paris Ufaransa.
19513984222_b5e615666b_o 
Baadhi ya washiriki wakiwa nje ya mkutano huo wakiendelea na shughuli wakati wa mapumziko...
19359209648_53d8f88215_oBaadhi ya Wanasayansi wakifuatilia mkutano huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.