YANAYOJIRI ZIARA YA RAIS OBAMA NCHINI KENYA


RAIS WA MAREKANI BARRACK OBAMA HII LEO ANATARAJIWA KUKAMILISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU NCHINI KENYA AMBAPO AMEWAHUTUBIA WAKENYA KATIKA UWANJA WA KASARANI NA BAADAYE KUELEKEA KATIKA CHUO KIKUU CHA KENYATTA ILI KUZUNGUMZA NA MAKUNDI YA WANAHARAKATI NA WANAFUNZI.
14.05pm:Habari njema nchini Kenya ni kwamba kuna katiba mpya ambayo inatoa mwongozo.Baadaye alifungua mjadala wazi katika kikao hicho.
14.02pm:Makundi ya kijamii yalijitokeza baada ya raia kujitokeza na kuanza kuzungumzia maswala yanayowaathiri
13.50pm:Obama awasili katika chuo kikuu cha Kenyatta na sasa anawahutubia viongozi wa makundi ya kijamii
Chuo kikuu cha Kenyatta University
13.00pm:Chuo Kikuu cha Kenyatta Jijini Nairobi
Obama
12.42pm:Obama amaliza hotuba yake kwa kusema 'Thank you Asante sana'
12.41pm:Amesema kuwa vijana wamemfanya yeye kujisikia nyumbani.
12.37pm:Ametoa changamoto kwa vijina kuchukua fursa iliopo ili kuiendeleza jamii huku akiongezea kuwa anahakika kwamba kenya inaelekea katika ufanisi mkubwa
12:35pm:Amewataka wakenya kutokubali kugawanywa katika misingi ya kikabila na kidini.
12:33pm:Amesema kuwa Marekani itashirikiana kwa hali na mali na kenya kukabiliana na tatizo la ugadi.'Magaidi ni waoga ndio maana hupendelea kutafuta makundi madogo madogo ya kijamii na kujaribu kuyagawanya''.Amesisistiza kuwa ugaid ni sharti ukabiliwe kwa hali yoyote.
12.32pm:Amesema kuwa ni sharti wanawake wapewe nafasi sawa katika jamii.'Udhalilishaji wa wanawake ni utamaduni ambao umekuwa tangu zamani lakini sasa hauna nafasi katika maisha ya sasa .Wanawake na wasichana ni sharti waelemishwa,Amesema kuwa kuna ufanisi mkubwa katika jamii ambayo imewaelemisha wanawake wake.Tuwape wasichana wetu elimu.Tunapowaelimisha wanawake tunawapatia nguvu kuzaa watoto walioelimika.
Obama kasarani
12.27pm:Amesema kuwa Marekani inashirikiana na Kenya kupitia uwekezaji wa vijana nchini.Amesema kuwa kila taifa lina utamaduni wake,lakini akaongeza kwamba tamaduni nyengine zimepitwa na wakati.Unyanyasaji wa kijinsia ni tamaduni zetu lakini ni lazima zibadilishwe.zinawarudisha nyuma.
12.25pm:Amasema kuwa harakati za kukabiliana na ufisadi lazima zianze kuanza juu na kwamba sheria za kukabiliana na janga hilo ni sharti ziwekwe,huku akiwataka wananchi kusimama kidete na kukataa ufisadi.
12.23pm:'Ufisadi ndio janga linalozuia mataifa mengi kupiga hatua'.Amesisitiza kuwa iwapo Ufisadi hautakabiliwa vilivyo utaathiri maendeleo ya taifa kwa jumla
Obama-kasarani
12.20pm:'Kwa ushirikiano wetu kuimarika ni sharti tuwe na taasisi zilizo imara katika uongozi wa taifa hili kwa lengo la kuimarisha demokrasia'.Amesema kuwa mara nyengine demokrasia huonekana kupendelea upande mmoja lakini sivyo akasisitiza.Amesema kuwa wanasiasa huwa na misimamo tofauti na hutarajia demokrasia itawapendelea na wasipopendelewa hulalama.
12.17pm:Amesema kuwa Marekani ni mshirika wa karibu na rafiki mkubwa wa Marekani na hivyobasi itaendelea na ushirikiano huo kupitia kuhakikisha kuwa kuna uongozi mzuri nchini Kenya.
Obama
12.16pm:Ugaidi ni swala jingine ambalo Obama anasema kuwa limerudisha nyuma maendeleo na kutoa heshima zake kwa wale ambao wamepoteza maisha yao katika kukabiliana na janga hilo pamoja na wale walioathirika.
12.15pm:'Siasa za kikabila na za kibaguzi hazina mwelekeo na hazifai kuendelezwa',alisema Obama
12.14pm:Ufisadi-amesema kuwa unafaa kukabiliwa kwa njia mbali mbali kwa kuwa unawadhulumu wakenya wa kawaida pato lao la kila siku.
Obama na Rais Obama
12.12pm:Alitoa sifa kwa marehemu Wangari Maathai kwa jitihada zake na ukakamavu wa kupigamnia demokrasia.
12.11pm:Amesema kuwa wakenya walikataa kugawanywa katika misingi ya kikabila huku sauti za viongozi na makundi ya kijamii yakisababisha kupitishwa kwa katiba mpya
Ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya
12.10pm:Alizungumza kuhusu vita vya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo nusra viangamize taifa la Kenya.
12.09pm:Uwezo wa vijana na maendeleo yaliopigwa na kenya ni fursa nzuri kwa vijana kujiendeleza wakati wowote.
12.06pm:Babu yangu alikuwa mpishi wa wakoloni.Obama alieleza vile alivyoweza kupata elimu.
12.04pm:'katika uwanja wa ndege mwanamke mmoja aliona jina langu na kuniuliza iwapo ninahusiana na Mtu anayemjua kwa jina Barrack Obama,na hapo ndipo nilijua kuwa jina hilo ni muhimu'
Obama
12.03pm.Obama anasema kuwa alipozuru kenya kwa mara ya kwanza alikula ugali na sukuma na pia alikuwa akilala katika kiti katika nyumba ya dadaake Auma.
Obama akiwasili
12.03pm:'Nakumbuka nilipokuja miaka 30 iliopita nilipoteza mzigo wangu katika uwanja wa ndege wa Jomo kenyatta ,lakini hilo haliwezi kufanyika katika Airforce one'.alisema Obama
Rais Barrack Obama na UHuru Kenyatta
12.01pm:Obama aingia katika jukwaa na kuwasalimia wakenya Habari zenu,wakenya mupo.Nafurahi kuwa wakenya kwa kuwa rais wa kwanza kutembelea kenya.Na pia kuwa mtu wa kwanza kutoka kenya kuwa rais wa Marekani,.
12.00pm:Auma amkaribisha Obama
The beast
11.58am:Amewachekesha wengi aliposema kuwa nduguye Barrack ambaye alimchukua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kwa gari aina ya Beattle takriban miaka 30 iliopita amerudisha hisani yake alipombeba ndani ya gari la the Beast wakati alipowasili.
11.56am:Auma amewakumbusha wakenya kwamba rais Obama yuko hapa kikazi licha ya kuwa mwana wa kenya.
11.53am:Awahutubia wakenya kuhusu dhifa ya hapo jana ambapo anasema kuwa rais huyo wa Marekani alikula vyakula vya aina mbali mbali vya kienyeji licha ya kukaa Marekani kwa muda mrefu.
Auma na dadaake bi Auma Obama
11.52am:Dadaake Rais Obama Auma Obama amepanda katika jukwaa kwa sasa
11.30am: Obama-Rais Barrack Obama wa Marekani pia amedaiwa kufika katika maeneo ya uwanja wa kasarani jijini Nairobi na wakati wowote kuanzia sasa atakaribishwa na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta ndani ya Ukumbi huo.
11.25am:Uhuru awasili Ukumbini
Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewasili katika ukumbi wa Kasarani
11.10am:Ukumbi wa Kasarani
Ukumbi wa kasarani
Ukumbi wa Kasarani ambapo rais Barrack Obama wa Marekani na mwenyeji wake wa Kenya Uhuru Kenyatta wanapaswa kuwahutubia Wakenya tayari umejaa mamia ya wageni waalikwa wakiwasubiri viongozi hao wawili.Tayari viongozi mbali mbali wakiwemo wale wa Upinzani wamewasili katika eneo hilo.
11.05am:Usalama Kasarani
Usalama K
Usalama
Usalama umeimarishwa katika uwanja wa Kasarani,ambalo ndio eneo ambalo rais Barrack Obama wa Kenya anatarajiwa kuwahutubia Wakenya
11.01am:Obama akicheza densi
Rais Obama
Rais wa marekani Barrack Obama siku ya jumamosi usiku alijiunga na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta katika chakula cha usiku na baadaye kucheza densi katika ikulu ya rais jijini Nairobi.
HABARI YA ASUBUHI -JUMAPILI TAREHE 26-JULY.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.