CHIKU ABWAO; UKAWA HAWANA NIA NZURI NA TAIFA HILI ,WATANZANIA KATAENI KUPELEKA IKULU WAFANYABIASHARA



                                                                        Bi Chiku  Abwao
 Na MatukiodaimaBlog
ALIYEKUWA mjumbe wa kamati  kuu Taifa  ya  Chama  cha Demokrasia  na maendeleo (CHADEMA) na mbunge  wa  viti maalum  mkoa  wa Iringa Bi  Chiku  Abwao amevitaka  vyombo  vya habari nchini kusaidia kuwaokoa  watanzania  juu ya kasi kubwa ya  wafanyabiashara  kung'ang'ania kwenda  Ikulu  kupitia vyama  vilivyokuwa vikiunda  umoja  wa katiba ya  wananchi (UKAWA)  kuwa kinachoendelea ndani ya  UKAWA ni hatari  kwa ustawi  wa Taifa na  sasa  limekuwa ni  genge la  wafanyabiashara .

Ambwao  ambae  alijiengua na Chadema hivi karibuni na kujiunga na chama cha ACT Wazalendo alitoa kauli  hiyo   wakati akizungumza na  wanahabari  mkoani Iringa  juu ya maandalizi ya  mkutano mkubwa wa ACT Wazalendo utakaoongozwa na kiongozi mkuu wa  ACT wazalendo  Zitto Kabwe  siku ya jumapili  wiki   hii.

Alisema pamoja na kuwa  dhamila ya  kukitoa  chama  cha mapinduzi  ipo kupitia vyama  makini kama chama  chake  cha ACT Wazalendo  ila bado  kuna njama  mbaya  zinazofanywa na vyama   hivyo zilivyojipachika jina la UKAWA kutokana na kuonyesha  kwao  wazi  wazi  kuwa wapo kimaslahi  zaidi  na  sio kwa ajili ya  kulikomboa Taifa  hili kwa  kupinga  ufisadi ila wapo kwa ajili ya  kusafisha na  kutetea vitendo vya ufisadi nchini jambo  ambalo ni hatari na  kuna  kila  sababu ya  vyomba  vya habari nchini  kusaidia kuelimisha  jamii ili  kukwepa kuingizwa  mkonge  UKAWA wanaokumbatia  ufisadi .

Alisema  kuwa  yeye  ni  miongoni mwa wanasiasa  wazuri   hapa  nchini ambae  kamwe hapendi  siasa  za maji taka  za  kukumbatia vitendo vya  ufisadi  bali  yupo kuona  anakemea na kupinga  kwa  nguvu  zote  vitendo  vya  ufisadi hapa  nchini  hivyo  hakupendezwa kabisa na hatua ya  CHADEMA  kumpokea waziri  mkuu mstaafu Edward  LOwasa kuwa  mgombea  urais  huku  wakitambua  wazi kuwa hana  sifa ya  kupinga ufisadi .

"Dhamira  ya  kukitoa  chama  tawala madarakani  ipo  lakini  kwa hatua  ambayo UKAWA  wameonyesha  ni kama  wapo  kwa ajili ya  kushangilia  vitendo vya  ufisadi  kutokana na  kukumbatia wale ambao  awali  waliwaita kuwa ni mafisadi papa  na leo wanatumia  nguvu  kubwa  kuuaminisha  umma kuwa ni  wasafi .......huu ni sawa na unafiki ambao  UKAWA  wameuonyesha na kamwe  itakuwa ni vigumu  watanzania  kuamini haya kwa  leo ......huyu  akiwa CCM tulipaza  sauti kuwa ni  fisadi leo amekuja  upinzani  tunauaminisha umma kuwa ni msafi .....hapana  hii si siasa ya  ukombozi kwa mtanzania  ila ni siasa ya  kibiashara  zaidi ambayo inafanyika UKAWA....nawaombeni  sana  wanahabari nchini msaidie  kuliokoa Taifa hili mhakikishe  kiongozi anayekwenda  Ikulu awe  mweye mwonekano wa kuliokoa Taifa   hili  si wa kwenda kutumia kivuli  cha  Ikulu  kuboresha biashara  zake  " alisema Chiku

Bi  Chiku  alisema Taifa  hili kwa  sasa limekwenda  pabaya kwani  limekwisha tekwa na wafanyabiashara na kuwa kwa upande wake  haamini kama  kweli kwa  viongozi wa Chadema wanania  nzuri na Taifa  hili kwa jinsi ambavyo  wanavyotangulia pesa  mbele na  kutaka  kuwaingiza kwa nguvu  kubwa wafanyabiashara  Ikulu.

" Hawa  Chadema awali  walikuwa mstari wa mbele  kukemea  ufisadi  ila  leo  wamegeuka na kukumbatia ufisadi na  kuwa chama cha kuwasafisha mafisadi kwa  kumpa nafasi ya kuwa mgombea urais  LOwasa na  kumuacha  Dr  Silaa ambae ni nembo ya siasa  za  Tanzania na nembo ya Chadema  .......Dr  Slaa ni   kiongozi  msafi na muadilifu anayetambua  kila mmoja wetu na  kuwa dhamira ya  kutaka  kuongoza nchi  yawezekana  wanayo ila  si dhamira  nzuri kwa  watanzania  wanataka  kutuuza  watanzania kwani  tutakwenda pabaya  kuliko hapa  tulipo"

Hata  hivyo  alisema kwa hali ya mambo yanavyokwenda  ni wazi  kuna  wakati mgumu  zaidi  kuliko  wakati  wote ule  uliopita kwani ni  mwaka  huu pekee ambao vyama vya upinzani vinakwenda katika uchaguzi mkuu kwa lengo  tofauti kabisa la  kuwapeleka wafanyabiashara  na  wachafu  Ikulu tofauti na awali  ambapo vyama vya upinzani kazi kubwa  ilikuwa ni kupinga CCM kwa ufisadi ila leo watanzania  wanashuhudia upinzani ukitetea  ufisadi .

Bi  Chiku  aliwataka  wananchi kuwa makini  na  mbinu  chafu ya UKAWA kutaka  kuliangamiza  Taifa   hili na  kuchagua vyama makini na  viongozi makini kutoka chama cha ACT wazalendo ambacho  ndicho  chama chenye sera na misingi  imara ya  kulikomboa  Taifa   hili  kutoka mikononi  mwa CCM.

Kwani  alisema hata  kinachotokea  ndani ya UKAWA kwa  sasa kwa  viongozi kujiuzulu nafasi zao ni sehemu ya pigo kutoka kwa mwenyezi Mungu kwa  kuona  wale  waliotumwa kuokoa  wakikengeuka na kuwa  waangamizaji  wakuu  wa Taifa  hili na kuwa hamshangi  aliyekuwa  mwenyekiti wa CUF Prof  Ibrahimu LIpumba na Dr Slaa  kujiuzulu nafasi zao kwani kama  wangebaki ni wazi  heshima  yao  ingeshuka  zaidi ya hapo na kuwa ndani ya UKAWA kuna  viongozi  wasiozidi  wawili ambao wanafanya siasa kuwa  biashara binafsi .

MWISHO

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.