Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya
urais, Bi. Samia Suluhu akiwasikiliza akinamama wakimuelezea kero ya
maji baada ya kumsimamisha na kumpa kero hizo Jimboni Longido.
Wakinamama wilayani Longido
wakiendelea kuteka maji kwa zamu baada ya kumaliza kumueleza kero zao
Bi. Samia Suluhu aliepita maeneo hayo.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa
Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza
nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa
Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza
nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa
Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza
nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwa katika vazi la kimasai alilopewa kama zawadi na wanaMonduli.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kampeni ya CCM taifa wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza Bi. Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa
Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza
nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Bi. Samia Suluhu akimnadi mgombea ujumbe wa Jimbo la Monduli, Bi. Namelok Sokoine (kushoto) kwenye mkutano wa hadhara.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa
Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza
nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
……………………………………………
Na Joachim Mushi, Longido
WANAWAKE wa Wilayani Longido
wamemsimamisha mgombea Mwenza wa urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi.
Samia Suluhu njiani akielekea jukaani kuhutubia wananchi wakimlilia
kuwatatulia kero ya maji katika Kata ya Longido ambapo kila familia
imekuwa ikipata huduma hiyo mara moja kwa wiki hali ambayo wamesema
haikidhi mahitaji.
Bi. Samia alilazimika kusimama
eneo ambalo wanawake walikuwa wamefurika wakichota maji kwa zamu huku
kila familia ikipewa idadi ya ndoo kumi mara moja kwa kila wiki kiwango
ambacho akinamama wengi walisema akikidhi mahitaji kwa familia zao.
Mgombea huyo wa CCM
aliwahakikishia akinamama hao kuwa yeye kama mwanamke anajua shida ya
maji inavyowatesa akinamama katika familia ikiwa huduma hiyo inapokuwa
tatizo katika upatikanaji wake, hivyo atalisimamia suala hilo. Alisema
Serikali ya CCM itakapoingia madarakani imetenga shilingi bilioni 13 kwa
ajili ya kupeleka maji eneo la Longido mradi ambao utamaliza kero ya
maji eneo hilo.
Akizungumza katika mkutano wa
hadhara Longido Bi. Suluhu alisema kwa kuwawezesha wafugaji wa eneo hilo
wamepanga kujenga mabwawa ya kuvuna na kuhifadhi maji kwa ajili ya
matumizi ya nyakati za ukame kwa baadhi ya maeneo, ikiwa ni pamoja na
kujenga majosho ya mifugo na kuwezesha madawa ya mifugo kwa wafugaji ili
kuwaendeleza.
“…Kazi hii tutaifanya ndani ya
kipindi kifupi mara tu baada ya kufanikiwa kurudi madarakani, Serikali
inayomaliza muda wake imefanya mengi na sisi tutaendeleza na kuboresha
zaidi. Alisema wanajua kilio cha mahakama katika wilaya ya Longido hivyo
mara baada ya kuingia madarakani wataijenga.
Alisema akiwa njiani katika
mikutano ya kampeni zake ameshuhudia uwepo wa ukame katika vijiji lakini
anawahakikishia hakuna mwananchi ambaye atakufa na njaa endapo hali
hiyo ya ukame itaendelea, kwani serikali ya CCM katika ghala la chakula
ina akiba ya kutosha.
Mgombea huyo mwenza wa CCM pia
alifanya mkutano wa hadhara katika Jimbo Monduli aliwaomba wanaMonduli
kumpigia kura ya ndio mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe
Magufuli ili aweze kutekeleza ilani ya chama hicho ambayo pia
imejumuisha ujenzi wa barabara ya Sanya Juu hadi Longido na Longido hadi
Mto wa Mbu wilayani Longido.
Aliwaomba wanaMonduli kumchagua
mgombea ubungw wa Jimbo la Monduli kwa tiketi ya CCM, Bi. Namelok
Sokoine kwani mgombea huyo anarekodi na historia nzuri ya utendaji kama
alivyokuwa babayake marehemu, Edward Moringe Sokoine. Aliwaomba pia
kuwachagua madiwani wa CCM ili waweze kufanya kazi kwa ushirikiano kama
timu.
Comments