MBUNGE
wa jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam,Mussa Hasan Zungu ameyaasa
makampuni yanayotoa huduma za simu nchini kuzidi kuzidi kubuni huduma za
kurahisisha maisha kwa wateja na kusogeza huduma zaidi kwa wananchi
ili wazipate popote walipo.
Zungu
aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa duka jipya linalotoa huduma
mbalimbali za Vodacom lililopo barabara ya uhuru Kariakoo katika
mwendelezo wa kampuni hiyo kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo
imefungua maduka katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam na
maeneo mengine nchini. “Nawapongeza kwa kusogeza huduma hasa katika
kipindi hiki ambacho sekta ya mawasiliano inazidi kukua siku hadi
siku”alisema.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema kuwa kampuni
imejipanga kuendelea kuboresha huduma zake na kuwekeza zaidi katika
kuimarisha huduma ili kuwawezesha wananchi na wateja kwa ujumla
kuzipata kwa urahisi.
“Sisi
kama kampuni tunaamini kuwa tumefikia mahali tulipo kutokana na wateja
wetu kutuamini na kuendelea kutuunga mkono na ndio maana nasi tumeamua
kutumia kipindi hiki kuwasikiliza vilevile kuwasogezea huduma karibu na
kwa mara nyingine napenda kusema Ahsante wateja wetu waliopo katika
mtandao wetu na wale ambao hawajajiunga na mtandao wetu tunawakaribisha
wajiunge ili waendelee kupata huduma bora”Alisema.
Ferrao
alizitaja baadhi ya huduma za kampuni hiyo ambazo zinaendelea
kurahishisha maisha kuwa ni M-Mpesa ambayo inategemewa na makampuni na
watu binafsi kutuma fedha na kufanya mihamala mbalimbali ya malipo kwa
hapa nchini na ikiwa tayari imevuka mipaka ya nchi bila kusahau huduma
ya Kilimo Klub ambayo imelenga kuwakwamua wakulima na kuwarahisisha
maisha na huduma ya kutoa mikopo nafuu ya M-PAWA vilevile alitangaza
kuzinduliwa kwa kifurushi kipya kinachojulikana kama Mpango mzima
ambacho kinatoa unafuu kwa wateja kupata huduma za data.
Baadhi
ya wateja waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo walisifu hatua ya Vodacom
kuzindi kusogeza huduma karibu na wananchi “Huduma hizi zikisogea
karibu nasi zinatupunguzia adha ya kutembea muda mrefu kuzifuata
nawapongeza Vodacom kwa kuwajali wateja wake”.Alisema Abdulqadir Rashid
mmoja wa wateja aliyefika dukani hapo.
Tofauti
na mwaka jana ambao kampuni ya Vodacom iliadhimisha wiki ya huduma
kwa wafanyakazi wake kushiriki katika shughuli mbalimbali za
kijamii,mwaka huu wafanyakazi na maofisa wa kampuni wameweza kukutana na
wateja na kuwaelimisha huduma mbalimbali za kampuni ikiwemo kusogeza
huduma karibu kwa wateja kwa kufungua maduka sehemu mbalimbali jijini
Dar es salaam na Masasi mkoani Mtwara.
Katika
mkoa wa dar es Salaam maduka ya Vodacom yamefunguliwa katika sehemu za
Ubungo,Mbezi Beach,Mbweni na kariakoo.Vodacom ina mtandao wa maduka ya
kutoa huduma kwa wateja zaidi ya 100 kwa nchi nzima.
Mbunge
wa Ilala jijini Dar es Salaam,Musa Hassan Zungu(kulia)akisisitza jambo
kwa Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(watatu toka
kushoto)wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kutoa huduma mbalimbali za
Vodacom Tanzania lililopo barabara ya uhuru kariakoo,wengine katika
picha wa kwanza kushoto ni Ofisa mkuu wa mauzo na Usambazaji Keith Tukei
na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.
Mbunge
wa Ilala jijini Dar es Salaam,Musa Hassan Zungu(kulia)akimsikiliza
jambo Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(watatu toka
kushoto)wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kutoa huduma mbalimbali za
Vodacom Tanzania lililopo barabara ya uhuru kariakoo,wengine katika
picha kushoto ni Ofisa mkuu wa mauzo na Usambazaji Keith Tukei na Mkuu
wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.
Mbunge
wa Ilala jijini Dar es Salaam,Musa Hassan Zungu(katikati)pamoja na
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto)
wakikata utepe kuzindua duka jipya la kutoa huduma mbalimbali za Vodacom
Tanzania lililopo barabara ya uhuru kariakoo,wengine katika picha
kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn
Mworia na Mteja wa kwanza kufika katika duka hilo,Abdulqadir Rashidi.
Comments