JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Nukushi: 255-22-2116600
|
|
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa
zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki au kujeruhiwa huko Saudi
Arabia
Mahujaji wengine wane (4) kutoka Tanzania ambao walikuwa miongoni
mwa wale waliokuwa hawaonekani tangu ajali ya kukanyagana kwa mahujaji
ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa
kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki
dunia. Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa
Tanzania waliopoteza maisha katika ajali hiyo kufikia thelathini na mbili (32).
Majina
ya Mahujaji hao kutoka kikundi cha Khidmat Islamiya ni:-
1. Abdul Idd Hussein
2. Adam Abdul Adam
3. Rashida Adam Abdul
4. Khadija Abdukhalik Said
Aidha,
hadi
sasa mahujaji saba (7) kutoka Tanzania bado hawajulikani walipo na jitihada za
kuwatafuta bado zinaendelea. Majina ya Mahujaji hao ni:
1. Burhani Nziru Matata
2. Farida Khatun Abdulghani
3. Juma Jecha Jaku
4. Laila Manunga
5. Nassor Mohammed Hemed
6. Saleh Mussa Said
7. Shabinabanu Ismail Dinmohamed
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
20 Novemba, 2015
Comments