MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA WAMESAINI MKATABA NA PSPF LEO JIJINI DAR ES SALAAM

 .Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF),  Michael Mhondo  akuzungumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani)  juu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wamesaini mkataba wa kutoa huduma za afya  kwa wanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari leo jijini Dar es Salaam
 Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF),  Michael Mhondo wakushoto na kulia ni Mkurugenzi wa PSPF Adam Maingu, wakisaini mkataba wa kutoa huduma za afya  kwa wanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari.  leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF),  Michael Mhondo na Mkurugenzi wa PSPF Adam Maingu,wakishikana mikono baada ya kusainiwa mkataba huo
Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF),  Michael Mhondo  na Mkurugenzi wa PSPF Adam Maingu, wakizidua huduma za afya  kwa wanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari.  leo jijini Dar es Salaam. 

MFUKO wa Pensheni  kwa Watumishi wa Umma(PSPF)  kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), wamesaini mkataba wa kutoa huduma za afya  kwa wanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa PSPF Adam Maingu alisema idadi kubwa ya wanachama  wa uchangiaji  wa hiari ni watanzania  ambao  wapo katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi kama waendesha bodaboda, mamalishe, wakulima, wafugaji, wasanii, wanamichezo na wajasiriamali.

Amesema baada ya kufanya utafiti waligundua kuwa  matatizo makubwa yanayowakabili  ni upatikanaji wa huduma za afya  hivyo wamekubaliana na mfuko wa bima ya afya kwamba mwanachama atakayelipia  kiasi  cha Sh 76,800 atatengenezewa kadi ya bima ya afya  na atapata huduma za afya  kwa kipindi cha mwaka mmoja chini ya udhamini wa PSPF.

“Walengwa wakuu katika fao hili la matibabu ya PSPF ni wanachama wa Mpango wa Uchangiaji  wa Hiari  na wategemezi wao watano  kwa kila mwanachama.

“Mwanachama wa PSPF atakayejiunga  na mpango huo atanufaika  na mafao yote  ya bima ya afya  sawasawa na mwanachama mwingine  yeyote wa  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

“Huu ni mpango wa aina yake  katika sekta ya Hifadhi ya Jamii  hapa nchini,  kwani mnufaika atapatiwa  kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  na kuweza kupatiwa huduma  ya matibabu  nchi nzima  kwenye vituo vyote vilivyosajiliwa na NHIF kuanzia Hospitali ya Taifa, rufaa, Hospitali za binafsi, mikoa, vituo vya afya na zahanati  zote za Serikali.

“Pia huduma hiyo itakuwepo katika vituo vya mashirika  ya dini na binafsi pamoja na maduka  ya dawa  yaliyosajiliwa na PSPF,”alisema Maingu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Michael Muhando, alisema  kusainiwa kwa mkataba huo utawanufaisha wananchi wengi waliojiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali vikiwemo vya umoja wa madereva wa malori, wavuvi, wakulima pamoja na vyama vya waandishi wa habari.

“Lengo ni  kuwajengea uwezo  wajasiriamali kuwa na maisha bora, na vikundi 38 tayari tumeshavisajili na mfumo wa awamu  ya tano  wa ‘Hapa kazi tu’  tunautekeleza kwa kasi” alisema Muhando.

Almesema mfuko wa NHIF ulianzishwa  kwa ajili ya  kuwezesha watu  kuchangia huduma za matibabu  kabla ya kuugua  na tangu  tangu mfuko huu ulipoanza shughuli zake mwaka 2001 umekuwa ukipanua wigo wake kwa kusajili  makundi ya aina mbalimbali  ili kufikia lengo la Serikali afya bora kwa wote

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.